dracular
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 769
- 1,061
Habari ndugu zangu wana JF,
Kama kichwa cha habari kinavojieleza,
Swala la ndoto ni kitu cha kawaida sana katika maisha ya mwanadamu, ndoto humtokea mtu pale anapokuwa amelala haijalishi ni mchana au usiku lakini ndoto ni ndoto tu, ndoto hizi huwa zimebeba ujumbe flani katika maisha yetu sisi wanadamu ambao anataka kutufikishia, hata katika vitabu vya dini inaaminika kwamba Mungu husema na watu wake kupitia ndoto hivyo basi ndoto si kitu cha kupuuza kwani ni kauli ya Mungu kwa mwanadamu.
Asilimia 99.9 ya ndoto aotazo binadamu ni za ukweli haijalishi umeota mchana au usiku. Tuna sema ndoto ni za uongo kwa sababu hatujishugulishi kuzitimiza kwa kuitii sauti ya mungu, mfano wewe umeota utakuja kuwa rais wa taifa lako alafu unaikataa shule au hutaki kujiunga na chama chochote cha siasa hapo utakuwa umeidharau sauti ya Mungu na ndoto hiyo haitakuwa kweli, tujifunze kuisikia sauti ya Mungu kupitia ndoto na tukazane kupambana ili kutimiza agano lake. Na kama ndoto ni mbaya basi tukeshe tukiomba na kusali ili Mungu aepushe hilo janga.
Mimi ni shahidi katika hili kwani niliota nitafaulu mtihani wangu wa kidato cha nne katika shule ilioko mkoa fulani ikabidi nikomae na kitabu ili ndoto iwe kweli na nikafanikiwa kwenda mkoa ule ule na shule ile ile not only that mimi matokeo yangu ya kwenda chuo hata kabla hayajatoka nilijua naenda chuo gani na tayari nilikuwa nimeshaanza kutafuta na chumba karibu na chuo na ikawa kweli cause niliota na ndoto nikaifanyia kazi.
Siwezi shuhudia ndoto zote hapa zilizokuwa kweli ni nyingi sana.
Ewe ndugu yangu mwana JF, hebu jifunze kuisikia sauti ya Mungu na kupitia ndoto na kuitii.
Huwa mnaota ndoto nyingi za ukweli ila mnazipuuza.
Ahsanteni sana.