Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
JAMANI MAPENZI.
Nifafanue mapenzi, nisemayo uchukue,
Kwa shairi si utenzi, nataka uyatambue,
Huenda bora utunzi, cha mno hoja ujue,
Twapenda wasotupenda, mapenzi ndivyo yalivyo.
Ni mchezo wa kukosa, hilo kwanza ulijue,
Si zamani hata sasa, si mzigo uutue,
Mawada ada kutesa, uchunge yasikuue,

Ni mchezo wa tanga, pepo yafuatilie,
Sifikirie ni nanga, baharini yanasie,
Penzi lataka ujinga, ndipo ulifurahie,

Si mchezo wa hisani, hakuna nipe nikupe,
Penda tena kwa imani, malipo yake matope,
Umuweke hata ndani, kumbe waishi na kupe,

Si mchezo wa usawa, hata kwa wapendanao,
Hakosi kuelemewa, mmoja kati ya hao,
Huba zikamsumbuwa, chungwa aone limao,

Mwisho mapenzi mchezo, usokuwa na sheria,
Pia hauna katazo, wala ya kushikilia,
Sema yataka chetezo, ubani kuyafushia,

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0762845394/0784845394 Morogoro
mzalendo.njano5@gmail.com