Habari zenu wana jf.....
Nina rafiki yangu ambaye ni msichana, kwa kweli ni mzuri sana na kama kajaliwa, kweli ni ka jaliwa kwa uzuri aliopewa na Mola, rafiki yangu uyu, yeye ni wa wale wa mura, ana mchumba wake ambaye nae ni mjita, na wanapendana sana.
Ila shughuli inakuja ni kwamba wamefanana sana kiasi kwamba kila atakaye waona pamoja hufikiri kuwa wao ni ndugu yani kaka na dada.
Sasa wameanza kuwa na wasiwasi wakifikiri kuwa kuna uwezekano wakawa ndugu ingawa kila mmoja ana baba na mama yake, Jamani wanaomba ushauri wenu wafanyaje?