Jamani hv kweli sina akili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani hv kweli sina akili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Abigree, Jan 19, 2011.

 1. Abigree

  Abigree Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kutokana na jinsi nchi inavyokwenda inaonesha watawala hawana akili,na wameweza kuwafanya watz pia kuwa hawana akili,wajione wasio na akili wala utamaduni,hata values mbele ya uso wa dunia.
  Swal linalonisumbua ni kwa sina akil km watz wengine? Km ninazo,nimefanya nn had sasa kuzdemostrate? Jibu la haraka na rahis n hakuna.
  Jaman,kwel jinsi mambo yanavyokwenda tz,maisha yanazd kuwa magum,watawala hawatuheshim,wanatunyonya,wanajinufaisha.
  Mim kama mtanzania halisi na halali cfany kitu kuokoa hal hii, kweli ninazo akili timamu mimi! Msaada jamani
   
 2. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Akili unazo sana. Ila umejaa woga wa kutisha. Usingekuwa na akili usingegundua matatizo uliyoyaeleza. Wewe ungeona yote sawa. Lakini kwa jinsi unavyonung'unikia matatizo yanayoletwa na viongozi wetu, hiyo ni akili tosha. Dawa ya kuondoa woga huu ni kuungana na wale wachache ambao wameonyesha ujasiri wa kuendeleza mapambano ya kukomesha maonevu, ufisadi na hujuma ya kila aina yanayofanywa na viongozi na mafisadi wa serikali lioko madarakani.
   
 3. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  siyo tu huna akili hata uwepo wako its b'se u think therefore u r!
   
 4. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ndio unayo akilia. Nakubaliana na mwenzangu. Tatizo nikwamba una uoga. Hutaki kusimama na kusema, 'Hapana inatosha.'
   
 5. Abigree

  Abigree Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nifanye nin bas ili huo uwoga unitoke, na nianzie wap au nifanye nin bas. Kwa kweli yatoshd, enough is enough
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Akili utakuwa huna. Ngoja nipitishe mchango tukuchangie akili.
   
 7. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,372
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Andika vizuri post zako kabla hatujajadili AKILI YAKO!
   
 8. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanaosema una woga wao hawana? Wamefanya nini ili na wewe ufanye?

  Unahitaji muamko. Au tuwakilishe wengine, nenda kwenye viunga vya ikulu jichome moto then sisi tutalianzisha kwa niaba yako!

  Vinginevyo, rudi kijijini kwako. Gombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji. Shawishi vijana wenzako wagombee vijiji vinavyounda kata yenu. Shawishi wengine wagombee kwenye kata zinazounda halmashauri yenu. Shawishi wengine wagombee udiwani kwenye kata zenu. Shawishi mmoja agombee ubunge. Ni kazi ya miaka karibu mitano kuanzia sasa. Unaowashawishi wawe wana uchungu na nchi yetu. Wawe waungwana na wasio na tamaa. Wawe wabunifu na wachapa kazi. Wawe wenye akili!
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  wengi kama wewe tunapenda kufanya mambo makubwa sana tena ya manufaa kwa jamii lakini jamii nzima ione na itambue nani aliyefanya hilo.
  Tanzania kuna wenye shida nyingi, wagonjwa, yatima, wajane, wazee, wafungwa etc.
  Hebu jitahidi kusaidia hapo hata kama ni msaada kiduchu.
  Neta hata hospitali wapelekee japo maji ya kunywa. Ni msaada kwakweli ingawa unaweza kuuona mdogo ila utabarikiwa.
  Usisubiri hadi uwe mbunge.
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni sawa kufanya kazi za kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa misaada. Lakini kuingia kwenye nafasi za uongozi ngazi za chini ni muhimu sana. Tofauti iliyopo kati ya Mbunge na Mwenyekiti wa kijiji kiuelewa ni kubwa mno kiasi kwamba unajiuliza wanawezaje kuwa na maono yanayofanana? Viongozi wengi wanawarubuni wenyeviti na madiwani kufanikisha wizi na udhalimu wao!
   
 11. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Tupo wengi waoga,akili tunazo sana tu............
  Dawa ya kutoa woga ni kupata uchungu kama huo ulionao,kuonekana mjinga,kudanganywa na kudhulumiwa.
  Tuungane na wasio waoga,tutapata nguvu ya kupambana vita dhidi ya mafisafi na wahujumu uchumi wote.:frusty:
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mkuu kila mtu ktk hii nchi anafikilia juu ya maisha yake na familia yake,ingawaje utofauti upo ukilinganisha na zama za kale kwani watu wa sasa wanauwezo hata wakusema kama wanaona mambo yanakwenda tofauti
  Akili unayo mkuu na nadhani upo mbioni kuamuwa jambo ambalo litaweza saidia kutatuwa matatizo tuliyonayo
  Pia tambuwa kuwa wabongo walio wengi wanatambuwa nini kinaendeleo tunasubili mtu wa kutufunga mabomu ili tuanze mchakato wa ukombozi na nadhani tumesha anza
  hivyo mkuu wakati ni huu wa kuweza kutafuta ufumbuzi wa matatizo uyaonayo hapa tz,ikibidi iwe kama TUNISIA

  MAPINDUZIIIII DAIMAAAAAA:frusty:
   
 13. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nina wasiwasi kama unazo, na kama zipo basi hazijatumika ipasavyo maana umeamua kuwa mdanganyika. Na kuhusu woga mimi nakataa, ni kwasababu tu hajanyonywa vya kutosha kuweza kusema basi. yaani kuweza kusema enough is enough.
   
Loading...