Ni hospitali gani hiyo?wakuu jana nilikwenda wapo mission wana kifaa cha kupima afya mwili mzima kwa sekunde 56 na kinakupa majibu yote nakama unaflash disk wanakuwekea majibu yako na pia wanamtambo wakutoa sumu mwilini hapo ndio waliniacha hoi kidogo wanakufunga belt kiunoni na mkanda mkononi kisha wanatumbukiza kiplastiki kmoja kwenye maji unatumbukiza miguu baada ya mda maji yanaanza kubadilika yanakuwa machafu kabisa ila kwenye vipimo niliweza kubaini ukweli fulani kwani nilitoka kupima full blood picture pale aar so nimewakubali
Ni hospitali gani hiyo?
Ni hospitali gani hiyo?
Na bei zao zikoje tafadhali tupatien detail zaidi.
Na hasa ikizingatiwa kuwa ni habari mpya machoni na masikioni mwa wengi humu jamvinihizo taarifa zitakuwa zimetusaidia zaidi
Na hasa ikizingatiwa kuwa ni habari mpya machoni na masikioni mwa wengi humu jamvini
Ndugu hata mimi nilikutana na vipimo hivyo wanavyo vya aina mbili lakini vyote vimekuwa computalized. kipimo cha kwanza wanakuchomachoma kwenye viganja siyo kuchoma mpaka damu itoke ila wanakuwa wanagusa viganjani computa inaonyesha kama tumboni kunamatatizo au kichwani au lolote. wanapima magonjwa yasiyohitaji damu. magonjwa kama vile ukimwi, malaria na mengineyo yanayohitaji damu hawapimi.
pili wanapima kutumia kifaa ambacho inakishika kama umeshikilia fimbo baada ya dakika kadhaa unafunguliwa kurasa kibao ambazo wanaweza kukupa kwenye flash au kukuprintia kama siyo nyingi sana.
mkuu kwa upande wa vipimo mimi na dada yangu tumewakubali. Ila kwa upande wa kutoa sumu wao wanaita detoxification hiyo hata mie na dada yangu tulitoa lakini sijajua kama ni kweli au la lakini tulipotoka tulijiona wepesi, usingizi mwingi zaidi na mengine machache. hivyo ndivyo nilivyoshuhudia.
Na mkianza ugua kansa msishangae :twitch::twitch: nyie kimbilieni kila kitu kigeni mnajua side effects zake??
Tupeni habari zaidi wadau, mtuelekeze ilipo. Mimi binafsi nadhani huu mwili umezidiwa na sumu za vyakula, pombe na pollution ya dar. Aisee ukombozi umekuja.!!
sio hosp mkuu ni kama kituo wapo pale kurasini ukishapimwa wanadawa zao sio zakemikali
basi tupe jina la hicho kituo na gharama zake pia......drphone unaturusha stimu sana wenzio.....unatupa details kwa uchoyo mno..