tunajali zaidi watoto mkuu
ndiyo maana nikakwambia dunia ya utandawazi ina mazuri na mabaya yake, we unapiga kelele matangazo internet je? hivi mtoto akitaka kitu atakosa kwenye internet?
sasa unazuiaje? hapo ndiyo challege ya sisi wazazi wa ujumla wake. kwa hiyo mtoa mada asishikirie matangazo ambayo mi naona si tatizo kubwa zaidi ya internet. ingawa mtu atasema watoto wangapi wana access ya internet makwao - lakini ambao hawana wanapewa story ya mambo yanavyokuwa, na kikawaida watoto wa rika moja wanaaminiana sana na kusikilizana. yule hana atawachukua wenzake awapitishe kwao wakaone wanachotaka.
So hili ni tatizo la ki- utandawazi, mtoto wa miaka 10 anajua hata process ya kuzaliana inakuwaje -
utandawazi hauzuiliki - na huwezi kuficha kitu na ndiyo maana wanakwambia anza kuongea na mwanao mapema. akiona tangazo la kama unampenda utamlinda - akiuliza mjibu jibu atakaloelewa kwa umri wake na ukimjibu HOVYO HOVYO ataenda kutafuta ushauri kwa marafiki zake shule.
its a challege to all of us - so what to do? u will never stop globalization my friend - never.
Matangazo ambayo ni kikwazo kwangu ni yale ya "kama unampenda utamlinda" hapo hata kama mtoto akikuuliza kidogo inaleta utata, lakini hili la maximo na chui acha watu wamchangamkie chui wao.jamani kunamatangazo yananikera sana kwani watoto wangu na wamajirani yamewaharibu kweli kweli lakwanza ni hili la zain linalosema weweeeeeee uhuru wa kuongea jamaa ananyuka anaanza kukata mauno kisawasawa sasa ukiwaona watoto walivyolikrem mwanzo mwisho nawanavyokatika yani ni balaa.
lingine ni hili la serengeti serengeti sasa nikiyatazama sioni yanamaana gani kulingana na wanachokitangaza au nikuteka umakini wa watu kwanza kama ndivyo walengwa wamekukuwa ni watoto zaidi
ebu tushauriane ili huu ni mtazamo wangu
Kunguruu wa Songeaaaaaaa
yani ww acha tu,mm nilimnunulia my gal vile vitabu vya kusoma vyenye picha nikaanza,bby say apple-apple,tukaendelea mengine nikafika hapa,bby say chita-eeeh mama serengeti serengeti,nikaduwaa kila nikimfundisha ananiambia mama uyu serengeti bwana sio chita
dah, kumbe binti amekuzidi maarifa kiasi hiki?/
kweli serengeti serengeti imeleta mambo.