NAFIKIRE
JF-Expert Member
- Sep 5, 2014
- 660
- 454
Wanajamvi wasalaam:
Baada ya salamu,nitoe pongezi zangu za dhati kwa wanajangwani kuchukua tena kombe la ligi ya vodacom Tanzania kwa Mara ya tatu mfululizo..kongole kwenu...
Ila dukuduku langu kubwa ni kilichotokea kwenye uwanja wa ccm kirumba jana yanga ilipokuwa ikicheza na mbao fc...
Nasema sikuamini macho yangu "kwamba" au "eti" timu kubwa kama yanga,wachezaji wake bado wanaamini mambo ya ushirikina kwenye mpira nasema bado siami kama kweli wachezaji wa kiwango cha kimataifa waende kwenye lango la timu pinzani kufukua " eti" kuna kitu kimefukiwa kinawanyima wasifunge goli...kweli jamani wa kimataifa tumeshafikia huko... mmmh! ....hii ni hatari sana kwa mustakabali wa maendeleo ya mpira wa miguu kwenye nchi yetu...na nitashangaa sana kama tff hawatalikemea vikali hili na kuchukua hatua..
Pili nilisikitishwa sana kuona wachezaji wa kimataifa wanakosa nidhamu...kitendo cha kumsonga tu refa kilinichefua sana...niseme tu Mimi ni mshabiki wa yanga kindakindaki lakini nidhamu mbovu iliyoonyeshwa na akina msuva na wenzake...wapenzi wote wa mpira tunatakiwa kuipinga kwa nguvu zetu zote..tff chukueni hatua kwenye hili...toeni adhabu Kali iwe fundisho kwa wengine...nitashangaa sana kama hamtalisemea hili..yule refa alionesha kiwango kikubwa sana cha uvumilivu..na alikuwa anatakiwa atoe kadi nyekundu kwa msuva na wenzake lakini akawa na hekima asivuruge mchezo.
Ninaomba tff irudie kuangalia ule mchezo na ichukue atua kwa kutoa adhabu kwa wote waliotaka kumdhuru refa na kuaharibu mchezo.wasalaaam