Jaman nahitaji ushauri kwa hili

x-pel

Senior Member
Joined
Mar 23, 2015
Posts
163
Reaction score
59
Habar zenu wana Jf,

Naamini mko salama na wengi sasa mshalala,

Mimi ni mgeni wa kuleta uzi humu ndani kwani huwa nasomaga tu.Kiukwel mim nilikuwa na mtu wangu kama mwaka hivi na tulishindwana kwani alinipiga kwa kosa la kutopokea sim na tabia yake ya umariooo kwani hajui bei ya hotel wala chochote zaidi ni kuniambia bby nimefulia leo nitoe. Baada ya kumchoka na tabia zake za umarioo nikamwambia kwa hizi tabia zako hizi naomba tuachane kwa amani kwani sion future,siku nikimpa wazo la biashara ili tuongeze kipato wala hajishughulishi nalo japo mimi na yeye ni waajiriwa.

Kiukweli nilimchoka sana na tabia zake za kuja kulala kwangu kila ajiskiapo.Kiulweli mimi licha ya ajira yangu niliongeza kitega uchumi na maisha yakaenda nilijitahi japo ya nyumba yangu ya kupanga nikafunga kiyoyozi maana hili joto la Dar si mchezo.Baada ya kufunga kiyoyozi mwanaume akadai nahongwa na mwanaume mwingine but ukweli ni kwamba mimi nilimweka wazi income yangu yote pamoja na matumizi kiukweli huwa nasave to the maximum.

Akaamua kunichuhuza na kichukua simu yangu aka kaa nayo siku tatu ili ajue kama nin mpango kando,but hakuambulia chochote sasa alipoirudisha simu nikamwambie aniache niendelee kusaka maisha badala ya magomvi na mimi sipendi ugomvi alikataa kuwa hawezi kuniacha.Lakini baada ya mabishano akapunguza mawasilino na akaanza kuwepa profile yake picha na mwanamke ambaya niliwahi kumhisi yuko naye nilivoona hiyo picha wala sikumuuliza siku ya siku kanipigia simu oooh! bby leo nimefulia nitoe mwisho wa mwezi natudisha basi kiubinadam tu nikamtumia kias cha pesa kwenye simu yake.

Ilivofika mwisho wa mwezi wa pili nikampigia kumuuliza vipi rejesho langu? Kabla sijauliza vile nikakutana na sauti ya kabintibnikamsalimia vizuri tu na nikamwambia naomba kuongea na mwenye simu alikataa na kudai yeye ndio mwenyesimu nilijaribu sana kumsihi anipe niongee na mwenye simu akanikatalia kiikweli nilikasirika nikamwambia "acha ushamba"naomba kuongea na mwenye simu maana hii dunia sio kipindi cha kugombana na mwanamke mwezio ni kuongea tu kistaarabu na kieleweshana Lool, acha bidada maneno yamtoke kama chiriku na matusi ni mengi sana na alitumia namba ya huyu x-wangu huyo kunitukana kwa sms.

Mimi sikufuta sms hata moja na sikumtukana kabisa zaidi nilimwambia natamani ungetumia maneno kuliko hizi sms,
kweli niliumia kwa matusi ya mwanamke mwenzangu na "nikaamua ile namba ya x-iliyotumika kunitukana niikatie R&B ili huyo x akamatwe na polisi ili afanyiwe mahojiano kwanini simu yake itumike kunitukana mimi.Kiukweli nataka waumie kama nilivoumia mimi na iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hii Iove jamani,niko sahihi kumfanya hivyo maana nimepanga kuitekeleza hili wazo ndani ya week hii.

Naombeni ushauri juu ya hili wazo langu jamani.Ushauri wa busara please
.`
 
Mm ningekushaur ila umarioo ndio tabia yangu...so acha nilale kisho utawapata washaur wazur🙂
 
Uko sahihi kabisa, ila kama vipi mpotezee tu uendelee na mambo yako. Dhambi zake mwenyewe zitamtafuna mbele ya safari.
 
Nia yako ni kuwaumiza kwa sababu walikuumiza..
Kwa kua ndio linalokupa amani yako fanya.
 
Nadhani jambo la maana hapo ni kuachana na ujinga,huna kazi ya kufanya wewe!!!!??

Umeishatambua hao ni wapuuzi yanini kuanza kupoteza muda nao??potezea.

Jitulize atakuja mwenye akili.
 
Usipoteze muda wako bure, shukuru Mungu kwamba amekufungua macho na kukuonyesha huyo ni mtu wa aina gani. Fanya yako achana naye kabisa.
 
shkuru Mungu kimesanuka mapema kuliko ingefikia hata hatua ya kuolewa na mtu asiyekupenda... nakushauri achana na ishu ya polisi,, we mpotezee tu wala usimuulize tena kuhusu heka yako..

Ubinadamu kazi... .endelea na mambo yako ila uwe na msimamo coz mchizi anaweza akarudi tena na kujifanya anaomba msamaha so ukiwa na roho nyepesi utajua mwenyewe
 
x-pel Umesema una kitega uchumi na kazi yako na maisha yanenda kwanini unapoteza muda na huyo jamaa?? Are you not busy enough to live your life do your job and forget the past? Instead you want to waste your precius time and more money to find the peace which is in you. Change your way of thinking and you will understand what I mean. kuwa bize na mambo yako unless you still love him na unataka kujiumiza zaidi
 
Last edited by a moderator:
Reactions: ral
Hongera kwa kuwa na mtazamo wa maendeleo. Futa namba kisha endelea na maisha yako.
 
Temana nao washamba hao

Ila waambie unawashtaki kwa matusi walokutumia ili akili ziwakae sawa

Next time acha kukopesha hovyo, ushajua jamaa mario kilichokufanya umpe hela nini???
 
Jaman nashukuru sana na naona mmekuwa positive niachane nao....nawashuru sana wana JF...ngoja nifanye ya msingi kwa kweli....niwatakien kaz njema na mishughuliko yenye marejesho kwenye hii siku.....!
 
Usipoteze muda wako kuhangaishana na watu wasio onesha uthamani maana kwao upumbavu umewajaa vifuani mwao...
 
Pole na pia Hongera! Kama nimekuelewa tayari ulishakuwa na maamuzi ya kachana nae na kusonga mbele na maisha yako. La msingi calm down JIAMINI UNAWEZA PEKE YAKO, JIPANGE kisha move on.

SAMEHE hicho kiasi as if ni sadaka then time will heal maumivu yako maana definitely lazima kuna wakati utahisi kawivu flani. That's life and remember NOTHING GET AWAY THAT WAS MEANT TO BE YOURS..
 
Si jambo la busara na hekima kugombana na mtu aliyevurugwa, huyo x wako kavurugwa remember what goes around comes around. Achana nae
 
mae hapo we dai chako achana nae huyo ukpata hela yako usiiache ikaenda bure kwa punda ambao hata kwao n mizigo ..coz mijanaume ya hvyo dawa yao ikupe chako tu then tia teke asepe
 
Achana nae na umwache na umarioo wake wew endelea kufight for your future
 
Just leave him and her and they will appreciate you, ni kwambie kitu binti ukimya unaongea kwa sauti kali na ya juu sana. acha usiongee kitu halafu utaona POWER YA UKIMYA.
 
Kaakimya na usirudie tena kudeal na mamario, nasema kila siku heri ufuge nyau atakulindia panya stoo kuliko hao wadudu, fanya yako na hakikisha uteteleki, pesa kitu gani bhana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…