Jakaya Kikwete kama Waziri wa Nishati na Madini alishasafishwa na ripoti ya 2!!!

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
13,495
29,859
I love this country!!!

Kwa bahati mbaya sana siku inasomwa Ripoti ya 2 sikupata fursa ya kuisikiliza!! Anyway, labda niseme sikutaka kuisikiliza! Binafsi huwa nasubiria ripoti kamili ili niisome kituo kwa kituo!!!

Baada ya kuisoma ripoti hiy kituo kwa kituo, nikagundua kwamba, wakati tunafikiria JK nae ana hatia kwa kusaini hiyo mikataba kama Waziri wa Nishati na Madini, kumbe Ripoti ya Profesa Osoro ilishamsafisha kitambo!!!!

Sehemu ya 5 ya Ripoti ya Profesa Osoro (Ripoti ya 2) inazungumzia Mikataba ya uchimbaji madini (Mining Development Agreements-MDAs).

Kipengele hiki kinaanza kwa kusema:
Mheshimiwa Rais,

Mikataba ya uchimbaji wa madini inafanyika chini ya kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini, Sura 123. Kwa mikataba iliyoingiwa mwaka 1994, mikataba hiyo ilifanyika chini ya kifungu cha kifungu 15 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1979 na kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 .
Hiyo mikataba ya 1994 ndiyo ambayo ilisainiwa na JK!!!

Na kwa maana nyingine, Profesa Osoro na timu yake ni kama wanataka kutuambia tusimsumbue sumbue JK kwani yeye alisaini kwa kutumia sheria ya Nyerere isiyo ya kifasadi!!

Nadhani hiyo wakaona haitoshi, wakaamua kumpamba lakini bila kumtaja jina! Hawa hapa tena:
Mgodi wa Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Kahama Mine Corporation Limited). Katika mkataba huu, Waziri wa Nishati na madini kwa jitihada kubwa alifanikiwa kujadiliana na kampuni hii na kuiwezesha Serikali kupata asilimia 15 za hisa katika kampuni za uchimbaji. Hata hivyo, mkataba huoulifanyiwa marekebisho mwezi Juni, 1999 na kusainiwa na Waziri wa Nishati na Madini aliyefuata, Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda.
Hapo Profesa Osoro naona anajaribu kutuambia ni namna gani waziri asiye na jina jinsi alivyokuwa "ame-figh"t kweli kweli kuhakikisha serikali inapata 15%!!!

Katika hali ya ajabu kabisa, akaja waziri mwingine ambae ametajwa LIVE kwamba ni Dr. Abdallah Kigoda! Huyu bila kujali "fight" za waziri asiye na jina akaamua kuhujumu "struggles" za waziri waliyeshindwa kumtaja!!!

Itoshe tu kusema kwamba, mawaziri wooooooooooooooooote waliopita nishati including Muhongo wa juzi juzi; hawa wametajwa kwa majina yao kasoro waziri mmoja tu... aliyesaini mkataba wa Bulyanhulu!!!

Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, ni JK ndie alisaini mkataba wa Bulyanhulu (am ready to be corrected). Kwahiyo waziri asiye na ajina ambae ali-struggle kweli kweli ni JK!!!!

Shikamoo JPM!!! Ama kweli hakuna kufukua makaburi hapa!!!!!
 
Saa wewe unafikiri kufukua makaburi ya rais wastafu ni mchezo. hata hivyo hakuna ill motive ila wapinzani wanataka kufanya siasa wakati jpm anafanya kweli.
 
Ujinga ni kufikiri kuwa mwizi anaweza kumhukumu mwizi mwenzie
 
Uko sahihi nakumbusha mwenye haki hata ukimzika kidole chake kitashuhudia. Tusubiri tu
 
Mkuu Katiba imempa kinga ya kutoshitakiwa Rais na Waziri asiye na jina.
 
f99316105350833945fde01ffec8ac0d.jpg
 
Back
Top Bottom