IBARA YA 1 YA RASIMU YA KATIBA YENYEWE
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.
Hivyo ndivyo inavyosomeka rasimu yenyewe. Kama jina la Zanzibar limebaki, na kama nchi zote bado ni huru, kwanini jina la Tanganyika life?
ANGALIA IBARA YA 3, IBARA NDOGO YA PILI.
(2) Siku Kuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a)Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
Disemba;
(b)Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12
Januari;
(c)Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili;
Kama tunaita Tanzania bara itakuwa na maana ya kuikiuka Katiba kabla hata haijapitishwa kwa 7bu Ibara ya 3(2)a ni sawa na kuadhimisha cku ya taifa lililokwisha kufa!
Na kwa mujibu wa Ibara ya 3(2)c haioneshi kuwa kuna SHIRIKISHO LA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR bali Tanganyika na Zanzibar.
Je, Mh Jaji Warioba anataka kututengenezea nchi ya 3? i.e Tanganyika, Zanzibar na Tanzania Bara
TUNAITAKA TURUDISHIWE TANGANYIKA YETU.