Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman Atoa Siku 7

Mbassa

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
278
163
Jaji Mkuu Mohamed Chande
Othman Atoa Siku 7 Kwa Mahakimu
508 Watoe Maelezo Kwanini
Wasifunguliwe Mashitaka Kwa
Kufanya Kazi Chini Ya Kiwango.
JAJI Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othuman ametoa
siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo ni kwanini
wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya
kufanya kazi chini ya kiwango.
Jaji Mkuu Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar
es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.
Alisema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo
Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi
chini 100 mwaka jana.
Alibainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya
Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu wa
Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka
jana.
"Ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi
kwenye mahakama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi au
waliokwenda masomoni katikati ya mwaka au likizo za ujauzito
hawatahusika katika sakata la kujieleza.
"Majaji Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuainisha
mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango cha kesi
walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa mwaka jana na
kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa nini
wasichukuliwe hatua," alisema Jaji Chande
Jaji Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo,
ambapo walizitaka idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe
kimekamilika ili ijulikane ni hatua gani wanachukuliwe.
"Mahakama haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi.
Hakimu hatakiwi kufanya hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo
naazimalize. Haiwezekani katika mahakama moja hakimu mmoja
anamaliza kesi 800 mwingine anamalizia chini ya 100 hilo
halitakubalika kutokana na kasi ambayo tunayo," alisema
Jaji Mkuu Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika
kamati zao kwa hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni
kupeleleza, kuchunguza na kushughulikia mashtaka yote ya
nidhamu ya mahakimu.
"Mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi
na kushindwa kutoa sababu za kuridhisha kwa nini wameamua
idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa
haraka na Kamati za Maadili za Mahakimu kwa mujibu wa sheria
na taratibu za haki," alisema
Hata hivyo, Jaji Mkuu Chande alitoa pongezi kwa mahakimu
ambao wamevuka kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua
zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana na mahakimu wengine
wamesikiliza kesi 915,789 na 778.
Alisema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza,
kwa sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa
zikimaliza kesi na kuanza mwaka upya.
Jaji Mkuu Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo
zilianza na kesi 34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi
20,431. Kiwango cha kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi
zilizosajiliwa 2015 ni zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya
Mkuranga asilimia 141, Rufiji asilimia 121 na Bukoba Mjini
 
Back
Top Bottom