Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
KUFUKUZWA NDANI YA CHAMA....
Hata kama ingelikuwa ni Ulaya, dhana ya uanachama kwenye vyama vya siasa ni ile ile, HIYARI! Na kwa hiyo vikao vya chama fulani vinapomchukulia mwanachama wake hatua za kinidhamu, ni jambo la ndani ya chama na mwanachama asiporidhika zipo taratibu za ndani ya chama za kufuata na ama utaratibu wa kisheria nje ya chama, ikiwa anadhani ameonewa.
Na ili taasisi kama vyama zidumu, lazima uwezo na maamuzi ya vikao vyake vya ndani uheshimiwe na usiingiliwe. Mimi pia, ni muumini wa hatua za ndani za kitaasisi, siamini eti taasisi zitakuwa salama kwa kulazimishwa kufuga maradhi au kuendesha mazungumzo na watu ambao wanaonwa kwa jicho la usaliti ndani ya vyama vyao.
Ndani ya chama chako unapoonwa kama msaliti, hata kama wewe si msaliti, usalama wako na mafanikio yako ni vipaumbele, ni bora kuwa nje ya chama/taasisi husika kuliko kuwa ndani huku huaminiki na hutoweza kurudisha hadhi yako.
Vyama vyote vya siasa duniani hufukuza vinapoona ni wakati wa kufanya hivyo, ila hapa Tanzania, mwenye haki ya kufukuza ni CCM, wengine wakijaribu wanalazimishwa wazungumze na wasaliti wakubwa, kwa manufaa ya CCM.
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].