Iwapo CHADEMA haitawafukuza Wabunge Viti Maalum 19, nitajiondoa CHADEMA na kujiunga ACT Wazalendo

Godfrey-K

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
1,925
3,670
Kuna dhana imejengeka kwa baadhi ya wana chama katika chama chetu cha chadema kuwa viongozi wamekijenga chama zaidi kuliko ya wanachama hii si kweli, chama chetu kimejengwa na kila mwanachama kwa kadili alivyojaliwa.

Nikili kuwa Mimi ni mmoja ya watu walikijenga chama kwa nguvu zangu zote hadi kufikia kufukuzwa kazi kwa kuwa tu nipo upande wa pili. Misukosuko ilikuwa mingi, uhamisho kila siku, kuviziana kila siku hadi nikafukuzwa kazi. Yote haya nimeafanya si kwa kutegemea malipo Bali Imani yangu juu ya chama hiki nikiamini kuwa kitapigania haki na Uhuru wa wananchi.

Haya yaliotokea kwa akina Halima mdee ni kutuvunja moyo sisi wajenga chama, hivyo ili kuendelea kutupa nguvu sisi wanchama wa kawaida, tunaomba wote waliokula kiapo wafukuzwe Mara moja ndani ya chama chetu. Iwapo itakuwa kinyume, basi nitajiondoa chadema na kujiunga na chama cha ACT wazalendo.
 
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa CHADEMA Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama.

Baada ya sauti hizo kuvuja mara moja chama kilitangaza kikao cha dharura cha kamati kuu kuwahoji ili waweze kuchukuliwa hatua kali sana ikiwa pamoja na kufukuzwa a CHADEMA.

Matokeo yake baada ya kikao cha kamati kuu hao wabunge wauaji walisamehewa na kutakiwa kuomba radhi tu!

Kama hali ni hiyo, wabunge wa viti maalum a CHADEMA si wauaji na wala hawajatishia kumuuwa mtu yoyote ila wanajaribu tu kutumia haki yao ya kikatiba iweje wafukuzwe a CHADEMA?

Kweli kuwa mwanamke a CHADEMA ni dhambi kubwa kuliko wapanga mauaji waliosamehewa??

Tusubiri na kuona kesho kikao cha kamati kuu chadema kitaamua nini ,bila shaka Mbowe is going to be tested again na maamuzi tofauti na kufukuza yatamwimalisha ,na maamuzi ya kufukuza hao wanawake itakuwa ni kiss of death kwa Mbowe na a CHADEMA kwa ujumla.
 
Nakumbuka hata kiongozi wa mbogamboga alishawahi kutamka kuwa dawa ya msaliti ni kuuawa. Wasiuawe wafukuzwe tu chama wahamie CCM.
 
Watafukuzwaje wakati wana baraka zote za chama? Makamanda kuweni wapole tu msije mkajitundika bure.
 
Back
Top Bottom