iUshauri Mitsubishi Pajero GDI io

Huntsman

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2012
Posts
648
Reaction score
621
kwa wanozifahamu hizi gari ushauri wenu tafadhali je, ni gari reliable hasa kwa safari za hapa na pale na pia kwenda nayo mikoani? Ninapanga kununua hii gari hivyo naomba ushauri wenu wadau mnaoifahamu specs zake ni Engine in cc 1800 na transmission ni Manual.

Thanks in advance
 
Mimi nina pajero GDI 3.5l 6 cylinder ni gari nzuri sana ina starehe kuendesha nishawahi kuendesha from J'burg - Dar mara 2 bila shida yeyote. Inahitaji kuservice GDI pump kila 25,000km na kwa bongo chagua petrol station za kujaza kwani nyingi za petrol stations zina mafuta machafu yanayozibisha GDI pump. Mimi ninapendelea kuweka mafuta katika vituo vya Puma ma Total
 
mkuu nashukuru kwa experience yako makini na nitaifanyia kazi japo mimi nataka kununa ile GDI io 1.8 L 5doors. wenye exeperience zaidi na magari haya toeni uzoefu wenu tafadhali na ushauri juu ya matunzo kama mdau hapo juu.
 
mkuu nashukuru kwa experience yako makini na nitaifanyia kazi japo mimi nataka kununa ile GDI io 1.8 L 5doors. wenye exeperience zaidi na magari haya toeni uzoefu wenu tafadhali na ushauri juu ya matunzo kama mdau hapo juu.

Mkuu hizo nasikia huwa ziningua sana gearbox
 
this is the worst nightmare car you could possibly buy..... the engine is troublesome..... itaanza kuchemsha bila sababu... inazima bila sababu na kukuthibitishia hilo hapa bongo zinauzwa bei rahisi sana coz a lot of pipo walionazo wanataka kuziuza ingawa si rahis kuuzika maana wengi wanazijua udhaifu wake... kama unataka SUV check suzuki au RAV 4 kama mfuko hauruhusu cheki saloon cars tu!!
 
mkuu nashukuru kwa experience yako makini na nitaifanyia kazi japo mimi nataka kununa ile GDI io 1.8 L 5doors. wenye exeperience zaidi na magari haya toeni uzoefu wenu tafadhali na ushauri juu ya matunzo kama mdau hapo juu.
Huntsman ushauri wa damian marijani ni kama universal kwa gari zote za mitsubishi. they are very delicate when it comes to where you fuel and what type of fuel you load in the tank kwa maana ya quality also when it comes to service you have to be cautious sana na pump + plugs.
Ukifatisha hayo hakuna usumbufu wowote utakaoupata. Am telling you.
Go ahead
 
Last edited by a moderator:
Hiyo gari ni pasua kichwa labia ubahatishe kila Siku ni mafua tu
 
Hao wote ni waongo pasua kichwa tu, hiyo gari ninayo mwaka wa 4 sasa, tangu niagize toka Japan ingawa ni ussed, lakini tangu niichuue haijawahi kuniletea tatizo lolote zaidi ya kubadilisha engine valve moja ilikuwa imepinda. Mpaka leo nasafiria mikoni, mimi nipo Arusha, nilishaenda nayo Nairobi, Dar, Tanga na Mbeya. Safari zote hizo haijawahi kuniharibikia hata siku moja tena ni gari inayotulia sana barabarani,sana sana utabadilisha tairi tu kwa pancha, kitu ambacho ni cha kawaida katika gari. Cha msingi tunza gari yako,kama alivyosema Damin Marijan epuka kuchanganya vituo vya mafuta, jitahidi utumie kituo kimoja tu. Nakutakia kila la kheri.
 
Kaka hizo gari ni majanga, ni nzuri kuendesha kwa kuwa zinakimbia sana na zina raha yake na ziko juu popote unapasua but zikianza kupiga chafya ni balaa. Naongea coz ninayo, spea zake ni bei mbaya. Kupata mpya mtihani na ukifanikiwa kuipata basi ni ya uhakika hutasumbuka kuisaka tena na used ni kuanzia laki na kupanda juu. Kwa mfano niliwahi kununua sterling pump kwa laki 4. Fundi umpate anayezijua lakini hawa wa kuganga njaa wanaiua moja kwa moja na kuthibitisha hilo wapo mafundi wanazikimbia wenyewe hata ukitangaza dau kubwa. Sikushauri kununua na hapa nilipo yangu nasaka mteja.
 
Daaah wakuu nashukuru kwa chqngamoto zenu na mawqzo yenu constructive ila mimi hii nilitaka niagize Japan na milleage yake iko below 70000 km hapo vipi kuna unafuu maana napata mawazo yanayokinzana kidogo hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…