Mhadzabe
JF-Expert Member
- May 20, 2009
- 3,235
- 4,744
Kwanza kabisa niseme sina tatizo na uongozi wa ITV juu ya kuona haja ya kupata maono ya watanzania juu ya uongozi wa Mh. Rais Magufuli kwa siku mia moja kwa kuandaa kipindi maalam juu yake (labda kwa watazamaji wa tamthilia ya Stray cat wamekwazika maana umekula mda wao). Nina tatizo ya kujua hasa nini malengo ya kipindi hiki hasa baada ya kukifatilia mwanzo mpaka mwisho.
Baada ya kukitazama nimegundua kuwa hawakuwa na malengo hasa ya kuonesha watazamaji wake maoni yao juu ya uongozi wa Mh. Rais bali kufanya propaganda na kuendeleza kasumba ya kuymsifia mfalme pasipo kumweleza ukweli. Kwa mfano angalia mikoa ambayo Sam Mahela ameitembelea kupata maoni. Ni maeneo ambayo vyama vya upinzani hasa CHADEMA wamefanya vizuri. Mikoa hiyo ni pamoja na Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Geita na Kagera. Unaweza kujiuliza kwa nini wameamua kufanya cases zao katika mikoa hii na sio Dodoma, Rukwa, Tabora, Pwani au Zanzibar? Utagundua hapa wameichagua mikoa hii ili kuonesha watu kuwa maeneo ambayo CCM haikuungwa mkono wote wanamsapoti Mh. Rais.
Pili aina ya respondents wa mahojiano na mtangazaji wao wameonekana hata hawajui walichokuwa wanaulizwa. Kuonesha hilo ilifikia mtangazaji kuweka vipande vinavyoonesha eti wafuasi wa CHADEMA wanamuona Mh. Rais kama masia aliyeshushwa na MUNGU.
Tatu ,kazi ya kuedit maoni ya wananchi ilifanywa kimkakati zaidi. Eti kati ya waliohojiwa wote katka mikoa yote hawakuona mapungufu ya Mh. Rais! Hakuna raia hata mmoja ambaye aliona mapungufu ya rais kwa siku miamoja akiwa ikulu.
Nafikiri ITV mlikuwa na agenda nyingine na sio kupata maoni ya wananchi juu ya siku mia moja ya rais. Ni vema hata kama mnamikakati ya kumsifia mfalme ni vema mkawa smart zaidi na sio hii drama mlioiandaa!