mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 340
- 359
Wadau naomba tujadili pasipo jazba, katika siku za hivi karibuni nimekuwa nikifuatilia taarifa mbali mbali zinazorushwa na ITV ikikihusu Chama cha ACT wazalendo. Nilichobaini ni ama kwa makusudi au kwa kutokujua chombo hicho cha habari kimekuwa kikikihujumu Chama hicho, na nitatolea mifano michache juu ya hayo
Mwaka huu wakati chama hicho kilipokuwa kinafanya sherehe yao ya maadhimisho ya miaka miwili kule Zanzibar licha ya ACT kutoa msimamo wao wa kutoutambua uchaguzi wa marudio wa machi 20 mwaka huu, chombo hicho kilimtafuta mmoja wa viongozi na kuongea nae kuwa wanaitambua serikali hiyo
Pia katika siku za hivi karibuni Chombo hicho kimekuwa kikichukua taarifa za ACT na kuzichanganya na taarifa za vyama vingine kwa ajili ya kutafuta uhalali wa kuificha taarifa hiyo. Na jana katika hali ya kushangaza nimeshuhudia katika kituo hicho wakimtambulisha mtu anayeitwa Sabini kuwa ndiye katibu wa Itikadi na mawasiliano wa ACT Taifa badala ya Ado Shaibu na kisha mtu huyo akatoa tamko lisiloeleweka
Katika hili Chombo hicho ni wazi kina mkakati wa makusudi wa kuwahujumu wenzao kwa maslahi wanayoyajua