Mnyanyembe wa Mboka
JF-Expert Member
- Feb 10, 2017
- 2,348
- 3,036
Mimi ni mchoma mahindi wa huku kwetu Unyanyembe, katika kona moja ya mtaa mkubwa unaotokea kituo kikuu cha mabasi yaendayo DSM
Upeo wangu kielimu ni darasa la Saba "B" katika shule moja huku kwetu Kwihala, sehemu za Unyanyembe, Mboka Manyemaaa!!!
Hoja yangu, kwakua Nchi hii ni ya watanzania wote na si ya mtu binafsi, na kila mtu anahaki sawa kama mwanachi mwingine, na ikitokea haki zitatofautiana lazima tofauti hiyo itakua imeanishwa aidha kwenye kanuni au utaratibu wa sheria zinazo endesha Nchi.
Na sheria hizo lazima zitakua zimejadiliwa kwa mtazamo wa kina miongoni mwa wawakilishi wetu (Wabunge) wanao tengeneza chombo chakutunga sheria (Bunge) ili kuondoa migongano kati ya kundi au mtu, kuona kanyimwa haki dhidi ya kundi au mtu mwingine, na pia kuweka misingi na uratibu wa maisha ya kila siku kwa mazuri ya kufuata na mabaya ya kuacha au kukemea.
Nimesema hayo kwa kuona kua serikali ya wamu ya tano imekuja na mkakati mzito na wa maana sana pengine kuliko kitu chochote katika kupiga vita na kujaribu kutokomeza kabisa UJINGA na UMASIKINI. katika vita hiyo kuna silaha kubwa zilizo tumika ni kama ifuatavyo:
1. Imeanzishwa Kampeni ya kitaifa kuhakiki vyeti vya kugushi miongoni mwa wananchi wakiwemo wanafunzi na watumishi wa idara mbalimbali za serilikali na hata sector binafsi
Hapa tumeshuhudia makumi kwa mamia ya baadhi ya wananchi na watumishi wa idara za serikali walivyotaharuki kwa zoezi hilo adhimu, na hata kupelekea wengine kupoteza nafasi zao za kazi kwa kuwajibishwa au kuachia ngazi wenyewe. Na wengine kutiwa hatiani na hatimae kukabili adhabu zilizo endana na kosa hilo.
2. Pia kuna Kampeni ya Kitaifa kuhakiki watumishi wa idara mbalimbali za serikali wasio na sifa za utendaji kulingana na ngazi ya taaluma inayo endana na viwango vyao vya elimu walizo nazo
Hapa tume shuhudia makumi kwa mamia ya watumishi wa serilikali walivyo adhirishwa licha yankulitumikia taifa katika nyadhifa zao mbalimbali na kuchangia maendeleo ya nchi, lakini bado wamebezwa na kuonekana ni vituko na hata wengine wamediriki kukimbia nyadhifa zao kwa aibu, licha ya kua wamelitumikia taifa kwa muda mrefu, tena bila ya kujali chagamoto mbalimbali
3. Pia kuna Kampeni ya kitaifa kuhakiki wafanyakazi na watumishi hewa katika idara mbalimbali za serikali
Hapa tulishuhudia wakuu kadhaa wa idara za serikali wakiwajibishwa bila ya kupoteza wakati kwa kuchelewesha kutoa taarifa za watumishi hewa katika idara zao. Tuliona jinsi MKUU WA MKOA SHINYANGA MAMA MALECELA, ALIVYOWAJIBISHWA KWA JAZBA ZA MKUU BILA YA HURUMA WALA AIBU, licha ya Mama yule kua amelitumikia taifa hili kwa muda mrefu sana na anamchango mkubwa katika ujenzi wa taifa hili.
4. Silaha nyingine iliyotumika ambayo haikua nzuri na ilileta simanzi na majonzi makubwa katika jamii, hasa familia nyingi zilizoguswa moja kamoja na silaha hii mbaya inayo uwa bila huruma, pia imeumiza na kuchosha nguvu na rasilimali za watu HII NI SILAHA MBAYA KABISA KUWAHI KUTUMIWA DUNIANI dhidi ya vita vya kuutokomeza UJINGA na UMASIKINI
Hii silaha ambayo ilikuja pale Wizara husika na Taasisi zake kutangaza majina ya wanafunzi wasio kua na sifa za kujiunga na vyuo vikuu, licha ya kua walishadahiliwa, na tayari wengine walikua wameanza masomo,9 na wengine walikua wanakaribia kumaliza mwaka wa mwisho wa masomo yao.
Lakini bila ya huruma, hali yakua hawakufeli kwa kupata kiwango cha sifuri, bila ya kuangalia utendaji wao huko vyuoni pengine walikua ni watendaji walio tukuka pia, kulingana na nafasi zao za uanafunzi, lakini pia kama watoto walio jiepusha na dhahma za kukaa kijiweni au kua wakabaji au wezi au makahaba na kuamua kwenda kusoma ili walijenge taifa lao, dhambi hii ya kunyanyasa watu kielimu haito liacha taifa hili miaka mia.
Lakini cha ajabu licha ya ukali wa vita hiyo ya kupinga UJINGA na UMASIKINI, leo hii Mkuu wa Mkoa wa DSM, ambae imethibi kwa kiasi kikubwa kua emegushi vyeti kwa kua jina lake halisi ni Daudi Bashite, ambapo mpaka sasa ameshindwa kukanusha jambo hilo, na hivyo vyeti ni feki na ndio vilivyompelekea kupata elimu ya chuo kikuu kwa hila.
Eti kwa sababu tu ni Mkuu wa mkoa, ambae ana kiherehere cha kumuweka karibu na mkuu wanchi, eti pia ameonekana kuwa ni mtendaji alie tukuka katika wadhifa wake, japo mpaka sasa sijui wamepima utendaji wake kwa mizani gani, licha ya kua kampeni zote alizo anzisha zimefeli na hakuna hata moja iliyo fanikiwa.
Sasa basi kwa msingi huo ili kuondoa migongano miongoni mwa jamii ya watanzania, naomba dhamira ya makusudi inuiwe ili vyombo vinavyo husika vianze mchakato wa kutunga sheria itakayo wasafisha WAHALIFU au WATUHUMIWA hasa wa kugushi vyeti au wa makosa mengine, waweze kusafishwa kwa kuangalia matendo yao yaliyo tikuka, pamoja na uthubutu makini kulingana na eneo, cheo, wadhifa, taaluma, itikadi, mapenzi, majukumu au dhamana walizo nazo katika jamii.
Mfano: Mzee Nguza Viking (Babusea) anaetumikia kifungo cha maisha gerezani yeye na familia yake, Kwa kesi ya kubaka. Tunaweza kumsafisha kwa utendaji wake na uthubutu wake wa kupiga gitaa la solo kwa umahiri mkubwa, kiasi ambacho miziki yake mpaka leo haijachuja, kwa kuburudisha watu katika Bar mbalimbali, katika maeneo mbalimbali ya nchi. Hivyo mtu kama huyo tunaweza kumtukuza kwa nafasi yake katika sanaa ya muziki wa dansi, ambayo ameitumikia vilivyo nakuiletea sifa nchi hii katika tasnia ya sanaa ya muziki wa dansi.
Na ikiwa hilo litapingwa basi iundwe sheria ya kinyume chake kuwa
"Utendaji uliotukuka na uthubutu katika jamii kulingana na nafasi ya mtu hauto kua sababu ya kusafisha UHALIFU wa mtu husika"
... na badala yake watu wajipange kisaikolojia kua wasitegemee utendaji wao kua kichaka cha kuficha maovu yao, kama ambavyo Mkuu wa mkoa wa DSM anaetumia vita ya madawa ya kulevya kama kimbilio la kuficha UHALIFU wake wa kugushi VYETI. Ambapo miongoni mwa wananchi kuna watu wanamsapoti na wengine tunampinga.
Hivyo basi shime wahusika aidha moja ya sheria hizo zitungwe ili kuondoa mgongano miongoni mwa jamii ya watanzania.
Nawasilisha Hoja
Huku nikiwa hasira sana juu ya dharau anayo tuonyesha Raisi dhidi ya Muhalifu huyu, huku akisimama majukwaani akidai kua anaendesha Nchi kwa kufuata misingi ya sheria
Wenu Mnyamwela wa Mboka
Mchoma Mahindi wa Unyanyembe
Mboka Manyemaaaaa!!!