Itikadi Zavuruga CHADEMA na CCM Segerea

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
ITIKADI za kisiasa zimetajwa kuzorotesha kasi ya maendeleo katika Mtaa wa Migombani, Jimbo la Segerea, mkoani Dar es Salaam, anaandika Pendo Omary.

Changamoto hiyo inakuja baada ya 22 Januari, mwaka jana kuapishwa kwa Japhet Kembo (Chadema), kuwa mwenyekiti mpya wa serikali ya mtaa huo.

Akizungumza na MwanaHALISI Online mapema leo, Kembo anasema “changamoto kubwa ninayokabiliana nayo katika kutekeleza ahadi zangu nilizoahidi wakati wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014, ni baadhi ya watu kutumia utofauti wa itikadi za kisiasa kukwamisha utekelezaji wa ahadi zangu.”

“Wapo baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika mtaa wangu hawataki kuchangia au kushiriki katika shughuli za maendeleo. Taarifa ninazozipata ni kwamba wanataka maendeleo katika mtaa wetu yakwame ili wananchi wasinipe nafasi ya kuongoza tena katika uchaguzi ujao,” amesema Kembo.

Kembo anasema wakati anagombea nafasi hiyo, aliahidi kuboresha usafi wa mazingira, ofisi ya serikali ya mtaa kutoa huduma bure bila malipo, kuitisha mikutano ya wananchi, kuboresha miundombinu na kuimarisha ulinzi.

“Mpaka sasa utekelezaji wa ahadi zangu unaendelea vizuri. Najivunia kuboresha usafi. Tayari mkandarasa wa kuzoa taka kwa kila nyumba kuchangia Sh 10,000 kwa mwezi ambaye ni Juza General Suppr ameanza kazi. Tumeboresha barabara inayoanzia Oil Com hadi Seminari na sasa nipo kwenye mchakato wa kuhakikisha barabara ya Mega hadi Pazi inaboreshwa,” amesema Kembo.

Pia, amesema tayari amefanikiwa kuanzisha vikundi viwii vya ulinzi shirikishi ambavyo vinafanya kazi ya kuhakikisha wakazi na wageni wanaoingia katika mtaa huo wapo sarama pamoja na mali zao huku kila nyumba ikichangia Sh. 10,000 kwa mwezi.
 
Dah aya bwana ila mkuu sio segerea pekee na hili ni kwa nchi mzima.
 
Kwani wakati anahidi si aliahidi kwa ilani yake? Sasa nini kinamsumbua kutekeleza? Ndo maana unaposema wenzako hawawezi si kwamba kuna sehemu ya kuchukuwa hela na kuwapa watu.

Na hiyo ni sehemu ya maisha ya siasa.
 
Ni kweli hata sie huku ulongoni jimbo la ukonga tumenyimwa barabara kwa sababu ya itikadi za kisiasa
Poleni sana sisi tumechagua CCM mambo yankwenda barabara kabisa lami na maji kwa mpigo. Next election hamtafanya Makosa tena
 
Hao wanaopinga maendeleo waendelee kwa nguvu zote, muda ukiisha wakae wajitathimini wamepata nini katika mpango wao.

Wengine tunajenga barabara kwa fedha zetu mfukoni.

Hayo ndo maendeleo
 
Ni kweli hata sie huku ulongoni jimbo la ukonga tumenyimwa barabara kwa sababu ya itikadi za kisiasa
Tunajifunza kutokana na Makosa Najua hamtarudia Tena Hilo Ni fundisho tosha kwenu na kizazi kijacho
 
Ni kweli hata sie huku ulongoni jimbo la ukonga tumenyimwa barabara kwa sababu ya itikadi za kisiasa
Hii ni hatar sana kwa mstakabali wa taifa mkuu kilie ama unaonaje mkuu. Maana kuna sehemu tungetakiwa twende kasi ya sana ila itikadi za kijinga zinaturudisha nyuma mno.

Hebu fikiria kuna sehemu bila kuwa na gamba la chama flan huwezi fanya biashara kwa raha kabisa. Hebu jiulize Ukitaka kupiga deal lifanikiwe ukiwa na gamba la chama flani basi mambo yananda sawa.

Naisi sasa tuwe wazalendo wakweli sasa mana naona maneno ya mbunge Lemma yalikuwa na maana pana kweli, "Bendera za vyama vyetu zisiwe na nguvu zaidi ya utaifa wetu".
 
Hasa maeneo waliochagua upinzani hali imekuwa mbaya sana kila mtu analalamika mbunge pia analalamika na wananchi pia wanalalamika
Kweli kabisa wanasahau siku zote ukiwa mmoja huwezi ona makosa uyafanyayo Bali mkiwa pande mbili lazima upate idea nzuri na hapo ndipo utagundua wapi unamapungufu na maendeleo yataonekana
 
Wananchi wa Segerea wanamkubali sana mbunge wao Bonna Kaluwa anafanya makubwa.. Watu wa mabondeni msimbazi walilia machozi mbele yake.
 
Back
Top Bottom