The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,147
- 20,079
Tatizo hao waalimu wa kujua kingereza hawapo!
Itabidi turudi shule kujifunza kingereza upya,walisikika baadhi ya watu waliokua kwenye show ya fiesta.
Hii ni baada ya umati mkubwa wa watu waliokuwepo kwenye show hiyo kuambulia patupu nyimbo alizoimba mwanamuziki wa kimarekani,T.I.,wengi wanasema waliambulia niga,mother fu...ker,yeah,bi.tch na kulaumu kwamba wamepoteza hela yao mtu mwenyewe waliemtegemea kaimba kingereza kigumu ile hatari.
Waalimu wa kingereza changamkieni fursa mfundishe kingereza cha T.I.
mimi kiingereza cha marekani huwa kinanipa shida hata aongee obamahao akina T.I wanaongea kiingereza cha mtaani....hata huko US walioenda shule hawaongei kama hao wa mtaani akina T.I na ukisikiliza kiingereza cha mtu alieenda shule hata UK ni rahisi kumuelewa kuliko wale wa mtaani wasiosoma.
Hahahaha ndio wanavyoongeaga state uku mi pia nikiongea wabongo hawaelewi wanasema naongea sifungui mdomo.
Si kwamba wabongo hawajui kiingereza bali kingereza matamshi yetu baadh ya maneno ni ngumu kuelewa hadi usikilize kwa makini sana.
heheh....maajabu hayaishi..''Yaani huyu high school drop out akurudishe darasani ili tu umwelewe!!!!?'
Hahaha... Hao waalimu wanaofundisha kiingereza wanatumia 90% ya mda wa kufundisha huku wakiongea kiswahili. Soma vitabu, angalia movie za kimarekani na jitahidi uongee na watu wenye weledi mkubwa kwenye American English.
Mbona Rasi simba yupo na mikanuni yake ya ajabu anafundisha kiinglishi cha T.I.