Amavubi;
Hii kitu iliwahi kunitokea mimi. Story yenyewe inakwenda hivi: Kuna kipindi nilikuwa naishi na binamu yangu wa kiume, ambaye umri we ni rika moja na Baba yangu mazazi (RIP) ,nadhani walikuwa wamepishana umri miezi isiyozidi 6 tu, baba yangu Aiwa ndiye mkubwa. Sasa ilitokea katika kutafuta maisha, binamu yangu huyu aliwahi kuishi pamoja na baba yangu kwa kipindi kirefu sana, alikuwa anamfahamu baba fika hata tuseme ingetokea akamkuta amelala kitandani na amejifunika shuka gubigubi, atamjua kuwa ni yeye hata bila kumuona sura.
Sasa ilitokea siku akanikuta nikiwa nimelala kitandani, akidhani kuwa nimesinzia kumbe nilikuwa macho, ila nilikuwa naonekana kama nimesinzia. Akaanza kuongea peke yake kwa sauti kama ya masikitko hivi, aliongea kwa kilugha maneno ambayo tafsiri yake ni hii "mmmh yaani watu huwa wanafanana duniani, yaani hata namna ya kulala!".Nilimwelewa alichomaanisha na namna alivyoguswa rohoni mwake hadi ikapelekea akatamka hayo maneno akidhan hamna anayemsikia!