1.Ist 2005 bei yake C.I.F(beforward) ni $ 3000x1771 (exchange rate ya leo-BOT)=5,313, 000
2.Kodi yake tshs= 4,090,000 (TRA)
3.Registration+Road licence=320,000(TRA)
4.Port charge =240,000(TPA)
5.Delivery order $70×1771=123,970(shipping line)
6.Clearing agent fee= 250,000
Jumla=10,336,970
kama kuagiza gari kwa sasa bei hiyo na kumbuka hapo hujaweka bima na hujachora vioo na kuweka ribiti ili kuwasupress wezi wa vipuli, pia bado hujafanya service ndogo ndogo(kubadili oil, oil na air filter. Hizo ni garama za kutoa gari pale bandarini na kuagiza tu. Pia kumbuka hujapigwa longolongo za clearing agent na gari imetoka bila any extra cost.
Je kuna show room gani utakuta gari kama unavyosema ist ya 2005 chini ya 10.5 kama ulivyojinadi. Lazima itakuwa ni ist itakayokufanya uwafahamu mafundi gereji wote wa Dar/mtaani kwenu.
Come with fact as above and prove me wrong comrade
Good boy.
Tupe mchanganuo mzima wa manunuzi kwa manufaa ya wana jukwaa.
Ingia web ya TRA kuna excel ya namna ya kupata kodi
jamaa kalipa 4m, mie nimelipa 2.8, pia rate yangu haikua 1771, mine was 1653
Ingia web ya TRA kuna excel ya namna ya kupata kodi
jamaa kalipa 4m, mie nimelipa 2.8, pia rate yangu haikua 1771, mine was 1653
Mkuu sema bhasi kiasi chako cha mwisho mimi napanda hadi 9mlns!!! Biashara ni mazungumzo hakuna haja ya kugombana
Nimeomba break down ya agency kunitolea gari Nissan Xtrail ya 2007 cc 2000 kunipa huo mchanganuo... Wataalamu msaada hapa tafadhali kabla sijawa Escrowed. Kachanganua kama ifuatavyo
TRA- 5,800,0000
Agency fee- 250,000
Port charges- 400,000
Shipping line- 180,000
Plate number- 40,000
Working money- 50,000
Total calculation= 6,720,000
Ingia web ya TRA kuna excel ya namna ya kupata kodi
jamaa kalipa 4m, mie nimelipa 2.8, pia rate yangu haikua 1771, mine was 1653
Plate number ni 30,000
Agency fee ina working money ndani yake huna haja ya kulipa working money. Unamlipa nani na kwa kazi gani?
Pili hiyo kodi mbona ni ya Xtrail ya 2005/2006 maana 2007 kodi yake imechangamka kidogo(7,628,662)
Asante mkuu kwa ufafanuzi kidogo... Vipi kuhusu hizo port charges na shipping line?! Are they equivalent to respective unit?!
Ist huwezi kulipa 2.8 acha uongo
Ingia web ya TRA kuna excel ya namna ya kupata kodi
jamaa kalipa 4m, mie nimelipa 2.8, pia rate yangu haikua 1771, mine was 1653
Ukoo wote unaohusu IST, SPACIO, RAUM, hakuna kodi ya 2.8m
Ist huwezi kulipa 2.8 acha uongo
Acha kupotosha ama makusudi au bila kujua na ubishi bila fact JF si mahali pake rafiki.
Exchange rate lazima itumike iliyotolewa na competentet authority ya nchi husika -BOT KWA TZ; as per East Africa Customs Management Act ) ambayo kwa leo rate ni 1772tzs/usd
Si kweli kodi ya ist 2005 ni 2.8M
hata kama exchange rate ingekuwa 1653tzs/usd; kodi yake kwa hiyo exchange rate ni 3.61422M (kulingana na hiyo excel sheet ya tra otherwise hujui kuitumia au hujui unachoongelea.)
Be GT as the motto of JF
Note: nimeamua kutoa ufafanuzi si kwa sababu nakujibu wewe ila kwa sababu nataka waTz wenzangu wajue ukweli
Mshana port charge zipo sawa ila hapo kwa shipping line sina uhakika. Ila hiyo bei ni reasonable kwa aina ya gari
Ndugu kuna wapikistani wameharibu bei za magari. Nimeagiza fleet ya corola runx zimefika hapa kwa 9.8m kwa kila kitu nimeweka sokoni kwa 10.5m lakni wapakistani wanauza kwa 10m katika showrooms yao. Hii biashara ishakua ya kisengenyaji. IST NDUGU kuagiza mpaka unaitoa ni 8.5 mpaka 9.5 m. Check again your burgaining. Hakuna gari unaweza kuingiza for less than 8m labda vile vitoi aka passo. Vitz. Ractis. Fun cargo.
Acha kupotosha watu rafiki. Hapa ni JF si kijwe cha kahawa hivyo ukiongea ongea fact na si maneno yasiyokuwa na kweli. Kuna watu hapa kwa taarifa hizi wanafanya maamuzi juu ya gari watakayoagiza toka nje. Sasa we kama utampotosha mtu ni 2.8 halafu gari inafika anakutana na 4M au 3.7 kulingana na exchange rate huoni utakuwa umesababisha mtu kushindwa kutoa gari yake bandarini na hatimaye kupigwa mnada/kuingia garama za storage wakati anatafuta pesa ya kujazia.
Act like a GT
hata kama ungekua umeiingiza leo kutoka japan huwezi kuoata 10.5 kwa ist, the maxmum unapata ni 7.5
Pitia pitia show rooms ili kujua bei za magari mkuu