Duduwasha
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 5,703
- 3,658
Kwa Mara nyingine tena vyombo vya habari vya kiarabu vimesema milipuko mikubwa mitano ilitikisa jiji zima na miale mikubwa ya moto kuonekana kila kona ya mji mashuhuda wamasema waliona moto na vishindo vya sauti ya milipuko njia ya luelekea uwanja Wa ndege Wa kimataifa Wa Damascus majira ya alfajiri. 3:25AM Thursday 27th April 2017.
Report zinasema ghara la kuhifadhia silaha na tank la mafuta yameharibiwa kabisa hilo ghala yawezekana kulikuwemo na vitu vya kulipuka vinavyodhaniwa ni silaha nzito. Milipuko imetokea baada ya lisaa limoja kipita ndege kutoka Iran ilipotua. Na kawaida huleta silaha kwa ajili ya kundi la lebanon Hezbollah.
Israel imesema haiwezi kusema chochote kuhusu iwe kukubali au kukanusha kuhusika ila imeendelea kusisitiza kuwa msimamo wao upo vile vile kuhusu usalama wao. Na hawatoacha kuzuia kuona Hezbollah wakisaidiwa silaha.
Raisi Putin aliomba chonde chonde nchi jirani ziache uchokozi kwani zitazidi kuchochea hali isitulie nchini Syria haijajulikana Kama Israel aliwataarifu Russia kabla ya kushambulia ila Israel na Russia wanamikataba yao kutokuingiliana angani na kufahamishana kwa kila jambo.
Syria imesisitiza kuwa mashambulizi hayo ni ya ndege kutoka Israel.