DesertStorm
JF-Expert Member
- Nov 22, 2015
- 3,005
- 2,409
Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Al Manar, duru ndani ya utawala wa Kizayuni zimefichua kuwa Israel ingali inatoa matibabu kwa magaidi wana Ojeruhiwa katika mapigano na vikosi vya Syria na waitifaki wake.
Aidha imedokezwa kuwa magaidi hao hasa wa kundi la ISIS au Daesh na wale wa Jabhatu Nusra, tawi la Al Qaeda, wanapata matibabu katika hosptilai za jeshi la Israel katika miinuko ya Golan. Mwezi Juni mwaka 2015 wakaazi Wasyria wa Golan walinasa magari kadhaa ya jeshi la Israel yakisafirisha magaidi wa al Nusra katika eneo hilo.
Aidha mwezi Juni mwaka 2014 Kikosi cha Umoja wa Mataifa katika mpaka wa Syria na Israel UNDOF kilifichua kuwa wanajeshi wa Israel wameonekana wakiwasafarisha magaidi kutoka Syria. Kikosi hicho kina jukumu la kusimamia usitishwaji vita wa mwaka 1974 baina ya Israel na Syria. Halikadhalika mwezi Desemba mwaka 2015 kulifichuka video iliyowaonyesha wanajeshi wa Israel wakiwasafirisha kwa gari la kubebea wagonjwa magaidi waliojeruhiwa nchini Syria.
Imedokezwa kuwa hadi sasa Israel imetumia dola milioni 13 kuwatibu magaidi kutoka Syria katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Serikali ya Syria inasema nchi za Magharibi na waitifaki wao katika eneo hasa Utawala haramu wa Israel, Saudi Arabia, Qatar na Uturuki ndio waungaji mkono wakuu wa magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya Rais Bashar al-Assad.
Source:IBN TV