Wakuu kwanza napenda niwapongeza Azam pamoja na simba kwa kuweza kufanya mikataba ya kibiashara jana yaani ya kuitangaza simba katika kipndi cha Azam Tv kiasi cha shs millioni mitatu hivi. Kilichonikasirisha zaidi ni leo katika taarifa ya habari ya channel ten kipndi cha michezo Rage ameongea kijinga kama si msomi na mwenye mtazamo wa kimaendeleo. katika maelezo yake amechanganua jinsi bajeti ya simba ilivyotunishwa na jinsi gani eti hiyo bajeti inavyotegemea mauzo ya fedha za Okwi. Yaani alikuwa akitoa povu na kusisitiza eti pesa za okwi zikifika tu eti simba itakiwa na excess ya shilingi milioni 30 sasa sikumuelewa alikuwa anamaana ya bilion thelathini au millioni thelathini?