Isimani, Iringa:Majambazi yateka mgodi, wapora mil 81/- na kujeruhi 9

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi wa dhahabu wa wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyakavangala kilichopo katika tarafa ya Isimani wilayani Iringa na kupora fedha tasilimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 na gramu 400 za dhahabu huku wakiwajeruhi watu tisa.

Majeruhi wa tukio hilo la uporaji ambao baadhi yao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wamesimulia tukio hilo lililotokea siku ya tarehe 9 mwezi huu majira ya saa moja jioni ambapo kundi hilo la watu walivamia mgodini hapo na kuanza kuwasaka watu waliowataja kwa majina na kuwalazimisha baadhi ya wachimbaji kuwaonesha walipo watu hao.

Baadhi ya majeruhi hao wameiomba serikali kujenga kituo cha polisi katika eneo hilo la mgodi ili kuimarisha usalama wakisema kuwa uporaji huo ulifanyika kwa muda mrefu huku kukiwa hakuna msaada wowote kutokana na eneo hilo kutokuwa na kituo cha polisi wala huduma ya mtandao wa simu hali iliyowafanya majambazi hao kufanya tukio hilo kwa muda wa zaidi ya saa kwakuwa walijua hawatabughudhiwa wala kufurushwa na vyombo vya usalama.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka waporaji hao tangu walipopata taarifa hizo hapo jana na kuongeza kuwa serikali inashirikiana na wachimbaji katika eneo hilo la Nyakavangala kuratibu ujenzi wa kituo cha polisi ili kudhibiti usalama wa eneo hilo huku muhudumu wa afya wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Bi Gloria Mnyonge akielezea hali za majeruhi hao.

Chanzo: ITV
 
3250776_3250348tmp35792793483img20150818081515jpegfe1a674ab2d4eb0a7b538ae2af314d0f1727800505jpeg8cadae045aa02724047807c0b466255a_jpeg22d3dc3fb8567999b41cea94e78f92ee
 
Awamu ya tano ni ya magumashi sana,dereva wa lori asikii tunapiga kelele nyuma
 
Mbona msukuma alisema iringa hakuna dhahabu? Ccm kweli ni vilaza
 
pistol.jpg

WATU tisa wamejeruhiwa vibaya baada ya majambazi walio na silaha kuvamia machimbo mapya ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Nyakivangala, Isimani wilayani Iringa mkoani Iringa na kupora zaidi ya Sh milioni 81 taslimu.

Pamoja na kiasi hicho cha fedha, majambazi hao wanadaiwa kupora dhahabu zaidi ya gramu 400, simu nne za mkononi na baadhi ya mali za wafanyabiashara katika eneo hilo linalokimbiliwa na wachimbaji na wachuuzi wa biashara mbalimbali.

Akizungumza na wanahabari jana, Mkuu wa Wilaya ya Iringa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Richard Kasesela alisema tukio hilo linalodaiwa kudumu kwa zaidi ya saa moja lililitokea majira ya saa nne usiku juzi.

Alisema majambazi hao ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa kukimbia muda mfupi kabla askari Polisi kufika katika eneo hilo lililopo zaidi ya kilometa 50 kutoka Iringa Mjini. Kasesela alisema taarifa za awali zinaonesha majambazi hao walikuwa wakimfuatilia mmoja wa wafanyabiashara wa madini hayo aliyekuwa na kiasi kikubwa cha fedha katika machimbo hayo.

Alimtaja mfanyabiashara huyo kuwa ni Mginya Paulo Dadaye (38), mkazi wa Morogoro aliyeporwa zaidi ya Sh milioni 79 baada ya kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwa ni pamoja na mikononi na miguuni.

“Walikuwa wakimsaka mfanyabiashara huyo kwa kuwauliza, kuwapiga na kuwapora wafanyabiashara wengine mpaka walipofanikiwa kumkamata, kumjeruhi na kumpora,” alisema.

Aliwataja wengine waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na Bakari Beka, Sungari Shija (24) mkazi wa Geita, Fadhili Nalinga mkazi wa Morogoro, Nsurwa Msanga (30) mkazi wa Bariadi na Odrick Michael (33) mkazi wa Ipogolo, Iringa.

Wengine ni Kitandu Mabula (27) mkazi wa Tanga, Danie Masegu (40) mkazi wa Simiyu na Elia Mushi (26) mkazi wa Moshi ambao wote wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Chanzo: HabariLeo
 
Back
Top Bottom