Nimeisikiliza mara 4 na hii hapa ni my honest finding.
Beat: Sina matatizo nayo! Kama ni kui-rate naweza kuipa >=75%
Chorus: Kwa maoni yangu staili ya mwenye chorus ingawaje ni unique lakini anatakiwa kubadilisha kidogo. Jamaa yupo almost flat...!
Kapata nafasi kubwa sana ya chorus lakini ni kama hakuitendea haki beat wala chorus yenyewe. Kutokana na staili yake, kukosekena na lyrics za maana kwenye chorus, huku akipewa muda mrefu sana kwenye chorus, kuna hatari mtu akaanza kusikiliza lakini akaishia njiani kabla hajafika sekunde 42 ambayo aliyesimama kwenye verse husika si tu kwamba ameitendea haki beat bali hata flow yake imesimama.
Ila kuna jambo hapa! Tuliokuwa na idea na how things work in studios tunafahamu kuingiza vocal studio ni kazi nyepesi sana kwa sababu kipande cha dakika 1 unaweza kutumia saa mzima kuingiza vocal lakini wasikilizaji wasifahamu!!
Namaanisha nini?! Ingawaje jamaa kwenye verse ametembea perfectly, I doubt ikiwa anaweza kutembea hivyo hivyo akiwa ameshika mic live! Na kama ataweza basi much respect... labda sio mtu wa mipombe wa misigara! Staili yake ya ku-flow na urefu wa verse unaweza kumfanya akate pumzi!
Lakini hata kama hilo sio tatizo, bado ingekuwa busara sana endapo urefu wa chorus ungepungua! Naona chorus (au sijui ndo verse ya kwanza) imechukua zaidi ya dakika moja huku kwa kiasi kikubwa akirudia maneno yale yale. Muda mrefu wa chorus (sio chorus ndefu) unahatarisha msikilizaji asifike dakika ya 1:45 ambayo jamaa kaitendea haki.
Nusu dakika ingetosha sana kwa ile chorus ili jamaa anayetembea na verse akaivunja verse yake into 2, verse ya kwanza akaanzia sekunde ya 55, kisha baadae jamaa wa chorus akaingia tena, kabla ya mchizi hajaingia kumalizia verse ya pili.
Hii ingesaidia, mosi, kupunguza muda uliotumika kupiga chorus huku akirudia yale yale (ingawaje penye good taste sio mbaya), pili, msikilizaji angemfikia aliyetembea kwa kizungu haraka sana na tatu, hii ingemsaidia sana hata kama anafanya live.
Halafu kuna technical issue ndogo. Kwenye bridge ya "I don't why...!" somewhere dakika ya 3:50 or sekunde chache kabla ya hapo, kuna gap kati ya chorus na hiyo "I don't know why...!" Mtu akisikiliza juu juu hawezi kugundua lakini lipo about nusu sekunde hivi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.