Ishakuwa kawaida simba kuporwa wachezaji wa kigeni kwasababu ya ubahili, hizi ndizo sajili zilizo walaza na viatu mashabiki wa Simba msimu huu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Miaka kama mitano hivi iliyopita kabla simba haijamilikiwa milele na kanji ilibidi itumike nguvu ya ziada kwa kutumia gharama kubwa kwenye sajili za wachezaji, matumizi, kununua uwanja, n.k. ili kuziasa imani ya wanasimba apewe timu na kweli alifanikiwa alipoinunua timu kwa bilioni 20 za kwenye bango kubwa.. Binti ushamtongoza kakupa ulichotaka kuna haja ipi ya kumotongoza tena ?, baada ya hapo zile mbwembe za kusajili wachezaji ghali zikaisha ghafala, kwa sasa timu imekuwa ni biashara kama zilivyo biashara zingine za bosi, inabidi kanunu ya "tumizi dogo faida kuwa kuba (kubwa)" ifatwe 😂😂 kwa sasa pale simba wachezaji inabidi wawe wa gharama za kawaida,,, hawa wazito wazito inabidi kwanza wabembelezwe bei zao zishuke, wasuburi mikataba yao iishe kwa kuogopa bei za kuvunja mkataba, kuomba mishahara yao ipungue, n.k. muda huo wa kuomba omba kuna timu zenye malengo huwa zinawapora simba wachezaji bila huruma, simba wanabaki kuhaha tu😂😂

.... Sajili zilizowalaza na viatu wapenzi wa soka Nchini Tanzania msimu huu.

1. 🇧🇫 Aziz Ki >>> Yanga
2. 🇨🇫 Manzoki >>> Dalian FC
3. 🇳🇪 Adebayor >>> RS Berkane

Alafu kuna mtu mzima na akili zake anaamini kwamba mchina kapasuka vibunda milioni 930 kumsajili Manzoki kwa miezi minne tu kisha Manzoki aje Tanzania, kwanini tusimuite KOLO😂😂😂 Milioni 930 hizo ni dau maradufu ya zile milioni mia nne na kitu ambazo simba walisanda.
 
Kuna vile vichambuzi maandazi wanavihonga viseme wamesajiri kumbe utapeli mtupu

Anza na yule wa visit Morogoro utaskia "sources zangu zinaniambia manzoki atakuja kesho jioni"

Kumbe wamebeba wanzuki.
 
Kuna vile vichambuzi maandazi wanavihonga viseme wamesajiri kumbe utapeli mtupu

Anza na yule wa visit Morogoro utaskia "sources zangu zinaniambia manzoki atakuja kesho jioni"

Kumbe wamebeba wanzuki.
bila kusahau kuongeza 0 kwenye mikataba na sajili
 
Ok, tumekusoma.!!
FbTr8kYXkAAvD7w.jpg
 
Makolo kolo muwage mnajua maana ya rumours ni tetesi, mtandao kama transfermarkt wanatumia rumours na sio mikataba ya kweli, kama unabisha tafuta hata kithibitisho chochote cha mkataba huo kwenye mtandao huo, kisha uweke hapa

Yaani Simba washindwe kutoa milioni 400 halafu mchina katoa milioni 900+ na mshahara safiii, mnavuta bangi za wapi kuota kwamba Manzoki aje Simba kupokea mshahara ambao haufikii hata nusu ya anaopokea huko China ?

Tumizi dogo faida kuwa kubwa ..... Msimletee masihara kanji aisee
 
Hao wengine nakubali ila kumsajili mchezaji kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki matokeo yake mchezaji kala hela ya pre season kala hela ya kwenda kucheza friends match mmebaki coco beach mna kula mchanga huku mkijiandaa na mechi ya simba ijayo kuwafurahisha mashabiki.
 
Makolo kolo muwage mnajua maana ya rumours ni tetesi, mtandao kama transfermarkt wanatumia rumours na sio mikataba ya kweli, kama unabisha tafuta hata kithibitisho chochote cha mkataba huo kwenye mtandao huo, kisha uweke hapa

Yaani Simba washindwe kutoa milioni 400 halafu mchina katoa milioni 900+ na mshahara safiii, mnavuta bangi za wapi kuota kwamba Manzoki aje Simba kupokea mshahara ambao haufikii hata nusu ya anaopokea huko China ?

Tumizi dogo faida kuwa kubwa ..... Msimletee masihara kanji aisee
Simba na yanga zinawafanya watu wasiwe na akili timamu mchezaji aache kwenda China kula hela za bure aje ateseke kisa simba ila yanga kweli akili zipo kwa watu wawili tu.
 
Back
Top Bottom