IS yashambulia kivuko cha Uturuki

IS yashambulia kivuko cha Uturuki

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
141009193003_islamic_state_640x360_ap_nocredit.jpg

Islamic state

Afisa wa ngazi ya juu kwenye mji wa mpaka wa Kobane nchini Syria amiambia BBC kuwa wanamgambo wa Islamic State wamejaribu kukishambulia kivuko cha mpaka na Uturuki lakini wakashindwa kukidhibiti kivuko hicho.

Khalid Berkel amesema kuwa wanamgambo hao wameshambulia mji wa kobane kutoka pande tofauti katika jitihada za kuuzingira kabisa ambapo wamepiga hatua kutoka maeneo ya mashariki kwa kutumia mabomu yaliyotolewa kwenye magari.

Wapigani wa kikurdi na wanajeshi huru nchini Syria wanasema kuwa wanahitaji kwa dharura silaha nzito.

Maelfu ya raia wamekwama kwenye miji wa kobane na umoja wa mataifa umeonya kuwa kutatokea mauaji ya halaiki iwapo mji huo utatekwa .

Awali wito ulitolewa nchini Syria na Iraq wa hatua za dharura kuchukuliwa dhidi ya wanamgambo hao.

Vyombo vya habari vinasema kuwa maafisa nchini Iraq kwenye mji ulio magharibi mwa Anbar wameitaka serikali yao kuomba msaada wa vikosi vya nchi kavu vya Marekani katika vita dhid ya ISIS.



Chanzo: BBC

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/10/141011_is_syria_kobane
 
You amaze me kwa ku post vitu vya maana constantly! Not mind numbing staff pamoja na ku mask identity!
 
These monsters except to get virgins one day in hell. ......there's no a bigger slave than a slave mind.

Turkey is NATO Member. i hope ISIS can not dare to mess up with, Likewise they didn't attack The Jewish State. ..Hope they Aware of any miscalculation may led to their greatest demise. ISIS do not have Plane, Helcopter, Map, they depend mainlyon Toyota trucks, Infantry and compass which helped them to know positions -South, North west and East. probably they attacked Turkey border accidentally.



141009193003_islamic_state_640x360_ap_nocredit.jpg
 
Back
Top Bottom