Iran yaapa kulipa kisasi kwa kuuliwa mwanasayansi wao

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,038
18,014
Iran italipiza kisasi mauaji ya mwanasayansi maarufu, shahidi Fakhrizadeh

Nov 28, 2020 04:51 UTC

Waziri wa Intelijensia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran italipiza kisasi kufuatia kuuawa shahidi Mohsen Fakhrizadeh ambaye alikuwa Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu katika Wizara ya Ulinzi ya Iran.

Jana Ijumaa alasiri, Fakhrizadeh aliuawa shahidi baada ya gari lililokuwa limembeba kushambuliwa katika mji wa Absard katika eneo la Damavand mkoani Tehran.

Kwa mujibu wa taarifa, awali gari lililokuwa limesheheni bomu lilirupika na kisha ufyatulianaji risasi ukafuata baina ya walinzi wa Shahidi Fakhrizadeh na magaidi.

Waziri wa Intelijensia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mahmoud Alawi ametoa taarifa ambapo amebainisha masikitiko yake kufuatia kuuawa kidhalimu mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu katika Wizara ya Ulinzi ya Iran na kusisitiza kuwa vikosi vya usalama vya Iran vimeaza kuwasaka magaidi mamluki waliotekeleza jinai hiyo na kwamba italipiza kisasi damu ya shahidi huyu azizi kwa wahusika na wasababishaji wa jinai hii.

Idara ya Habari katika Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema Shahidi Fakhrizadeh alijeruhiwa vibaya wakati wa mapigano baina ya walinzi wake na magaidi na kisha akakimbizwa hospitali na kufariki kufuatia majeraha yake. Shirika la Habari la Faris limesema watu watatu hadi wanne waliuawa katika mapigano hayo na wote walikuwa ni magaidi.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amelaani vikali hujuma hiyo ya kigaidi na kuongeza kuwa, kuna dalili nzito zinazoonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika katika mauaji ya Fakhirzadeh, ambaye pia alikuwa profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Imam Hussein mjini Tehran.

Gari la shahidi Fakhirzadeh katika eneo la mlipuko

Katika ujumbe kupitia Twitter, Zarif ameandika: “Magaidi wamemuua mwanasayansi maarufu wa Iran leo. Kuna dalili nzito zinazoonyesha Israel imehusika na ni ishara ya wanavyotapatapa wapenda vita.”

Zarif ametoa wito kwa jamii ya kimataifa, hasa Umoja wa Ulaya kusitisha udumakuwili wenye kuaibisha na kulaani kitendo hiki cha kigaidi.

Naye mwenyekiti wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Meja Jenerali Mohammad Baqeri amesema hujuma hiyo ya kinyama imetekelezwa na magaidi wanaofungamana na uistikbari wa kimataifa na utawala wa kishetani wa Kizayuni. Amesema ingawa mauaji hayo ni pigo kwa sekta ya ulinzi ya Iran lakini maadui wafahamu kuwa, njia iliyofunguliwa ma wasomi kama Shahidi Fakhirzadeh haiwezi kufika ukingoni.”

Baqeri aidha amesema ulipizaji kisasi mkali unawasubiri waliotekeleza ugaidi huo kwani watafuatiliwa na kufikishwa kizimbani.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Amri Hatami amesema Shirika la Utafiti na Ubunifu katika Wizara ya Ulinzi ya Iran, ambalo lilikuwa likisimamiwa na Shahidi Fakhirzadeh, lilikuwa mstari wa mbele kuunda vifaa vya kupima ugonjwa wa corona. Amesema pia alikuwa akiongoza jitihada za kuunda chanjo ya corona nchini na matokeo ya jitihada hizo yatatangazwa.

Huku akilaani mauaji hayo, Hatami amesema Fakhirzadeh alikuwa pia naibu waziri wa ulinzi, na mwanasayansi mashuhuri aliyekuwa na historia ndefu ya ubunifu na aliwapa mafunzo wanasayansi wengi kwa ajili ya ustawi wa kisayansi Iran.

Kwa mfano alihusika katika utumizi wa takenolojia ya miale ya laser katika kutambua ndege za adui pasina kutegemea radar.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran Ibrahimi Raeisi amesema 'wasaliti wanaofungamana na ajinabi na Uzayuni wa kimataifa wametekeleza jinai kubwa kwa lengo chafu la kuzuia ustawi wa kisayansi nchini Iran. Huku akiwapongeza wanasayansi wa Iran kwa kuimarisha kasi ya ustawi wa Iran katika sekta mbali mbali za sayansi, ikiwemo sekta ya nyuklia, Raeisi amesema kuuawa shahidi Fakhirzadeh hakutasitisha mkondo wa ustawi wa Iran.

4bvfc4e5f7741b1rvf3_800C450.jpeg
4bvf3484b9af411rviq_800C450.jpeg
 
Hawa nimewashangaa sana kutompa gari armoured na blast proof. Mtu mzito vile anatembelea gari kama hizi V8 za kawaida na wanajua wanasayansi wa kinyuklia ni target kubwa. Miezi michache baadae kuna watu watanyongwa kwa kesi hii.
 
Kwa mawazo yao walijua Israel taifa Teule hawawezi kuingia Iran na kuua.
 
Hawa nimewashangaa sana kutompa gari armoured na blast proof. Mtu mzito vile anatembelea gari kama hizi V8 za kawaida na wanajua wanasayansi wa kinyuklia ni target kubwa. Miezi michache baadae kuna watu watanyongwa kwa kesi hii.
Kama zile za pole pole V.80 sio
 
Hawa nimewashangaa sana kutompa gari armoured na blast proof. Mtu mzito vile anatembelea gari kama hizi V8 za kawaida na wanajua wanasayansi wa kinyuklia ni target kubwa. Miezi michache baadae kuna watu watanyongwa kwa kesi hii.
Upo sahihi!..Mara nyingi wanaofanya matukio kama haya ni wapinzani wa utawala husika ila wanakodiwa,wanapewa mafunzo na kulipwa kutekeleza hivi vitendo na mashirika ya kijasusi ya kigeni ya nchi adui/hasimu wa Iran.

Ila huu mtindo wa kuuliana wataalamu au watu mashuhuri sidhani kama huwa una matokeo chanya sana sana unazidisha uhasama, uadui na Ugaidi wa kimataifa.
 
Imeisha hiyo....Hao ndo Israel jalada lishafungwa Sasa anatafutwa mwingine.....na siku Iran atakapothubutu kurasha hata jiwe Israel ndo utakuwa mwisho wa Iran maana itapigika kwa nguvu kubwa Sana ....Iran na miaka na miaka anaapaga tu kuwa ataifuta Israel kwenye ramani lakini Cha kushangaza mpaka leo jamaa wapo na sana Sana ilani ndo aiona joto ya jiwe iwe Iran kwenyewe au nje ya Iran juz tu vinu vimeripuliwa Leo kauliwa mwanasayansi mkuu hatar Sana
Iran italipiza kisasi mauaji ya mwanasayansi maarufu, shahidi Fakhrizadeh

Nov 28, 2020 04:51 UTC

Waziri wa Intelijensia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran italipiza kisasi kufuatia kuuawa shahidi Mohsen Fakhrizadeh ambaye alikuwa Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu katika Wizara ya Ulinzi ya Iran.

Jana Ijumaa alasiri, Fakhrizadeh aliuawa shahidi baada ya gari lililokuwa limembeba kushambuliwa katika mji wa Absard katika eneo la Damavand mkoani Tehran.

Kwa mujibu wa taarifa, awali gari lililokuwa limesheheni bomu lilirupika na kisha ufyatulianaji risasi ukafuata baina ya walinzi wa Shahidi Fakhrizadeh na magaidi.

Waziri wa Intelijensia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mahmoud Alawi ametoa taarifa ambapo amebainisha masikitiko yake kufuatia kuuawa kidhalimu mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu katika Wizara ya Ulinzi ya Iran na kusisitiza kuwa vikosi vya usalama vya Iran vimeaza kuwasaka magaidi mamluki waliotekeleza jinai hiyo na kwamba italipiza kisasi damu ya shahidi huyu azizi kwa wahusika na wasababishaji wa jinai hii.

Idara ya Habari katika Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema Shahidi Fakhrizadeh alijeruhiwa vibaya wakati wa mapigano baina ya walinzi wake na magaidi na kisha akakimbizwa hospitali na kufariki kufuatia majeraha yake. Shirika la Habari la Faris limesema watu watatu hadi wanne waliuawa katika mapigano hayo na wote walikuwa ni magaidi.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amelaani vikali hujuma hiyo ya kigaidi na kuongeza kuwa, kuna dalili nzito zinazoonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika katika mauaji ya Fakhirzadeh, ambaye pia alikuwa profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Imam Hussein mjini Tehran.

Gari la shahidi Fakhirzadeh katika eneo la mlipuko

Katika ujumbe kupitia Twitter, Zarif ameandika: “Magaidi wamemuua mwanasayansi maarufu wa Iran leo. Kuna dalili nzito zinazoonyesha Israel imehusika na ni ishara ya wanavyotapatapa wapenda vita.”

Zarif ametoa wito kwa jamii ya kimataifa, hasa Umoja wa Ulaya kusitisha udumakuwili wenye kuaibisha na kulaani kitendo hiki cha kigaidi.

Naye mwenyekiti wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Meja Jenerali Mohammad Baqeri amesema hujuma hiyo ya kinyama imetekelezwa na magaidi wanaofungamana na uistikbari wa kimataifa na utawala wa kishetani wa Kizayuni. Amesema ingawa mauaji hayo ni pigo kwa sekta ya ulinzi ya Iran lakini maadui wafahamu kuwa, njia iliyofunguliwa ma wasomi kama Shahidi Fakhirzadeh haiwezi kufika ukingoni.”

Baqeri aidha amesema ulipizaji kisasi mkali unawasubiri waliotekeleza ugaidi huo kwani watafuatiliwa na kufikishwa kizimbani.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Amri Hatami amesema Shirika la Utafiti na Ubunifu katika Wizara ya Ulinzi ya Iran, ambalo lilikuwa likisimamiwa na Shahidi Fakhirzadeh, lilikuwa mstari wa mbele kuunda vifaa vya kupima ugonjwa wa corona. Amesema pia alikuwa akiongoza jitihada za kuunda chanjo ya corona nchini na matokeo ya jitihada hizo yatatangazwa.

Huku akilaani mauaji hayo, Hatami amesema Fakhirzadeh alikuwa pia naibu waziri wa ulinzi, na mwanasayansi mashuhuri aliyekuwa na historia ndefu ya ubunifu na aliwapa mafunzo wanasayansi wengi kwa ajili ya ustawi wa kisayansi Iran.

Kwa mfano alihusika katika utumizi wa takenolojia ya miale ya laser katika kutambua ndege za adui pasina kutegemea radar.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran Ibrahimi Raeisi amesema 'wasaliti wanaofungamana na ajinabi na Uzayuni wa kimataifa wametekeleza jinai kubwa kwa lengo chafu la kuzuia ustawi wa kisayansi nchini Iran. Huku akiwapongeza wanasayansi wa Iran kwa kuimarisha kasi ya ustawi wa Iran katika sekta mbali mbali za sayansi, ikiwemo sekta ya nyuklia, Raeisi amesema kuuawa shahidi Fakhirzadeh hakutasitisha mkondo wa ustawi wa Iran.

View attachment 1636754View attachment 1636755
 
Iran akipata nuclear technology na kuzalisha mabomu atakuwa mbogo North Korea wala haioni ndani. Hajawahi tokea kobe yeyote kuingia N.Korea eti kuua mtu. Pia Iran wana traitors wengi ndani kwao
 
Back
Top Bottom