Iran Iraq war

Yusomwasha

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Posts
2,092
Reaction score
844
Habari wadau hivi ni nini kilisababisha Iran Iraq na je ni nini ilisababisha Iraq kuivamia Kuwait?

Na pia ni nini ilisababisha Iraq kurusha scud Israel?
 
Iraq,Iran,Syria,Libya,Kuwait na saudia zina hazina kubwa ya mafuta baada ya urusi bilashaka,ambayo kimsingi nchi zoote duniani zinahitaji mafuta,Amerika na washirika wake waliweka utaratibu kuwa biashara ya mafuta lazima ifanyike kwa US dollar hiyo iliaza miaka ya mwanzo ya 70,Karibu nchi zote hizo zilikuwa na vibaraka wa nchi wa magharibi.mwaka 1979 kukatokea mapinduzi Iran Kwa kumwondoa Shaa kibaraka wa Us,mapinduzi hayo yalikuwa ya kiislam yenye msing wa kupinga namna Amerika na washirika wake wanavoinyonya Irani,kikubwa kilicho waudhi watu wa magharibi ni serikali ya ya Iran kutaifisha shughuri zote za mafuta na kuwa za serikali,huo ndo ulikuwa mwanzo wa vurugu,vikwazo vya uchumi.kipindi hicho saadam akili yake ilikuwa baado sana kwa nchi yake,magharibi wakamtumia Saadam Hussein ati Iran ilichukua sehemu ya aridhi toka Iraq hapo ndo vita ikapigwa kwa miaka 8,Saadam alipopevuka kifikra akaachana na vita na kutafuta suluhu na irani na mbaya zaidi akaanza kuuza mafuta kwa euro na curreny nyingine.Hapo ndo Amerika na washirika wake wakawa mbogo kwa kuharbiwa Deal
 
Umejitahidi kutuletea history, sasa endelea huumgogoro uliopo vp na isis wao vp historia yao mkuu?
 
Hakuna aliyekujibu! Kwa kifupi Iraq ndiyo iliyoanzisha vita. Sababu kuu ni kuwa iliiona Iran iko katika hali mbaya ya kijeshi baada ya mapinduzi ya 1979, kwani wanajeshi wake wengi aidha walikimbia au walinyongwa. Kwa vile kulikuwa na migogoro ya mipaka, Saddam akaona huo ni wakati mzuri wa kurudisha alichokiona ni ardhi yake. Pia alikuwa na tamaa ya kumega fungu jingine la ardhi ya Iran ambayo wanaishi Waarabu iitwayo Khuzestan kwa Kiajemi au Muhammara, kama Wairaq walivyoiita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…