MKomela
Member
- Jun 6, 2017
- 27
- 16
EWURA imepokea maombi ya IPTL kuongeza mda wa leseni kwa miezi 55, kuanzia tarehe 16 Januari 2017 hadi 15 Julai 2022.
Naomba ieleweke kwamba leseni ya kuzalisha umeme hutolewa na EWURA kulingana na pamoja mambo mengine Mkataba wa kuuziana umeme yaani Power Purchase Agreement (PPA) kati ya TANESCO na wazalishaji umeme.
PPA ya IPTL na TANESCO ilisainiwa mwaka 1995 kwa miaka 20 (from Commercial Operation Date (COD). Leseni ya sasa ya IPTL ilitolewa na Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1996 kwa kipindi cha miaka 21. COD ya mradi wa IPTL ilifikiwa mwaka 2002 na kuanzia hapo ndo miaka 20 ya PPA ikaanza kuhesabiwa.
Maombi yaliyoletwa na IPTL ni kuongeza mda wa leseni uweze kuendana na mkataba wa mauziano ya umeme. Maombi ya yaliyoko EWURA kwa sasa sio ya kuidhinisha PPA bali kuhaakikisha uzalishaji wa umeme ambao unafanyika na IPTL unafanyika kisheria kwa kupata leseni kutoka EWURA.
Kwa mujibu wa Sheria ya Umeme na Sheria ya EWURA, MEM, AG na TANESCO ni wadau ambao wameombwa na EWURA kutoa maoni yao kuhusu maombi haya. Wananchi pia wameomba maoni yao kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha Sheria ya EWURA na kifungu cha 8 cha Sheria ya Umeme. Kwa hiyo, ni vema watanzania wakatoa maoni yao katika kipindi hiki ili kuisaidia EWURA kufanya maamuzi sahihi.
Kutokana na mijadala mingi ambayo imeendelea kwa miaka kadhaa kuhusu mradi huu, maoni ya MEM, AG, na wadau wengine yanahitajika sana ili kufikia maamuzi sahihi. Kwa sasa, kila mtanzania mwenye maoni/taarifa za kupinga ama kuunga mkono ombi la IPTL anaombwa kuwasilisha EWURA kama tangazo linavyosema.