Tunaambiwa; hivi karibuni, zaidi ya dola za Kimarekani 120 milioni (taarifa nyingine zinataja dola 250 milioni), sawa na zaidi ya 194bn/=, zimechotwa kinyemela kwa ushirikiano kati ya TANESCO/IPTL, kutoka Akaunti ya Mfuko wa Akiba Maalum (Escrow Account) Benki Kuu (BOT) kwa matumizi yasiyojulikana.