Bintiwangara
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 551
- 287
Kama kuna kashfa iliyoyumbisha vichwa vya Watanzania na serikali yetu katika miaka ya karibuni, yenye kuumiza uchumi wa nchi kuliko zote, kashfa hiyo ni ile ya kampuni ya kufua umeme ya "Independent Power Tanzania Limited" – kwa kifupi, IPTL.
Kama kuna kashfa iliyo wazi kuliko zote, zaidi kuliko hata ile ya EPA; inayokumbatiwa na ambayo viongozi wakuu wa serikali wanaingiza vichwa kwa kujifarangua na kunywea hima kwa mishiko, kashfa hiyo haiwezi kuzidi ile ya IPTL.
Kama kuna uwekezaji wa kifisadi nchini; ambao mwekezaji hohe hahe anaingia na "brief case" – mkoba pekee, lakini muda mfupi anageuka bilionea kwa kutumia bure rasilimali za nchi yetu, na kuendelea kuchezea akili serikali kwa kiburi bila kukoma pasipo hofu na serikali ikanywea, uwekezaji huo hauwezi kuzidi huu wa IPTL.
Kwa yote hayo; kwa nini tusiamini kwamba nchi yetu inaliwa na wenye meno; tena kila mmoja kadri ya ukali wa meno yake?.
Mwanzo wa kiama
Julai 1994, aliyekuwa Waziri wa Mipango na Katibu Mkuu wa CCM, hayati Horace Kolimba, alifanya ziara nchini Malaysia ambako alizungumza na wawekezaji wa sekta ya umeme wa nchi hiyo, na kuwaomba waje nchini kwetu kuangalia uwezekano wa kuwekeza ili kupunguza tatizo la umeme.
Kweli, Agosti 19 mwaka huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mechmar, ambayo baadaye ilimiliki asilimia 70 ya hisa katika IPTL, Datuk Baharuden Majid, aliongoza ujumbe mzito kutoka Malaysia kuja kufanya mazungumzo na serikali yetu juu ya uwekezaji huo.
Walioshiriki katika mazungumzo hayo kwa niaba ya serikali, ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini wakati huo [na sasa Rais wa Tanzania],Jakaya Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Simon Mhaville, Kamishna wa Nishati Msaidizi, Esther Masunzu, na Msaidizi wa Rais Ali Hassan Mwinyi wa Mambo ya Uchumi, Dk. Juma Ngasongwa.
Viongozi na Watendaji Wakuu hawa wa Serikali, kwa nia njema na thabiti kabisa, waliukaribisha uwekezaji huo bila kujua kwamba hatimaye ungeingiliwa na "dumuzi" mharibifu kwa njia na mtindo uleule uliotumika kwa kashfa ya rada, Richmond/Dowans, EPA, Merementa, Deep Green na kashfa zingine nyingi kubwa nchini.
Mwezi mmoja baadaye, Septemba 1994, Mkataba wa maelewano [MOU] ulifikiwa na kutiwa sahihi baada ya kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuwa ulikuwa mzuri na wa manufaa kwa nchi, licha ya tahadhari kutoka kwa washauri wa Kisheria wa TANESCO – Kampuni za Acres [Canada] na Hunton and Williams [UK], kwamba uwekezaji huo ulikuwa hati ya kifo kwa sekta ya umeme na kwa uchumi wa nchi.
Ulaghai wa IPTL
IPTL iliundwa mwaka 1994 kwa ubia wa Kampuni ya Mechmar Corporation [Malaysia] Bhd, yenye kumiliki hisa asilimia 70; na Kampuni ya hapa nchini –VIP Engineering and Marketing Ltd [VIPEM], yenye asilimia 30 ya hisa.
Mwenyekiti Mtendaji wa Mechmar ni Tan Kean Wan, na Mkurugenzi Mtendaji ni Datuk Baharuden Majid; wakati mwanzilishi wa VIPEM ni hayati Bakri Somji, na kusimamiwa na mwanae, Riaz Somji wa Dar Es Salaam. Mkurugenzi mwingine wa Kampuni ni Ahmed Daya.
James Burchard Rugemalila, aliyewahi kuwa mtumishi wa Benki Kuu nchini [BOT] wakati mmoja, na kuacha kazi kutafuta "malisho mabichi" au ya kijani, alifanikiwa kuwa mmoja wa Wakurugenzi wa VIPEM na Mkurugenzi wa IPTL kwa wakati mmoja. Aliingizwa VIPEM kutokana na kufahamiana na vigogo wa BOT na Serikali kurahisisha "maelewano" na utawala wa nchi.
Tumeandika mengi na mara nyingi, namna IPTL ilivyoingia mkataba tata na serikali yetu kupitia TANESCO, na jinsi nchi inavyoumia chini ya Mkataba huo hadi sasa.
Kwa kifupi tu; tumeandika kuonesha namna tulivyouziwa mitambo chakavu, hafifu na aghali kuendesha aina ya "Medium Speed Diesel" [MSD], badala ya mtambo uliokusudiwa kwenye Mkataba, aina ya "Slow Speed Diesel" [MSD]; na jinsi mradi mzima wa ununuzi wa umeme [PPA] na Ujenzi wa Mradi [EPC] ulivyoongezwa thamani kinyemela bila uhalisia kwa zaidi ya asilimia 133, na bei ya kuuziana umeme kuongezwa kwa asilimia 33% zaidi [kuwa senti za Kimarekani 13 kwa uniti moja] na kuwa umeme ghali Afrika Mashariki nzima.
Jambo hili lilisababisha TANESCO kufungua kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji [International Centre for Settlement of Investment Disputes] - ICSID mjini London, ambayo katika uamuzi wake, Februari 2, 2001; iliona kuwa, IPTL waliongeza bei ya umeme na thamani ya mradi kinyemela na bila ya uhalali wowote hivi kwamba, walitakiwa kuirejeshea TANESCO fedha waliyolipwa kutokana na ulaghai huo.
Kwa mujibu wa hukumu hiyo, ICSID ilielekeza TANESCO iendelee kujadiliana na IPTL juu ya bei sahihi ya umeme kwa kuzingatia gharama halisi ya mradi ya dola 123.5 za Kimarekani, badala ya dola milioni 163.0 zilizowekwa na IPTL, na kuikosoa IPTL kwa kitendo chake cha kihujuma, cha kubadili kinyemela mtambo wa technolojia bora wa SSD na kuuza hafifu wa MSD kwa bei ya SSD.
Ulaghai zaidi uliobainika ni pamoja na kuongezwa kinyemela kwa bei ya jenereta na mifumo saidizi, kutoka dola za Kimarekani milioni 51.7 mwezi Februari, kuwa dola 60.4; Matenki ya kuhifadhia mafuta, dola milioni 3.6 kuwa dola milioni 5.7; na kazi za ujenzi mdogo mdogo za kuusimika [Civil Works], kutoka dola milioni 5.6 kuwa dola milioni 10.0.
Nyumba 37 za ghorofa tatu kila moja, zilizopangwa kujengwa pale Tegeta kwa dola milioni 7.6, zilipunguzwa kinyemela kuwa sita za ghorofa moja moja, lakini kwa gharama hiyo hiyo ya dola milioni 7.6.
Aidha, mtambo wa SSD ambao TANESCO waliambiwa gharama ya dola milioni 163, ulibadilishwa na mtambo hafifu wa MSD, Desemba 1997, lakini kwa bei hiyo hiyo; wakati nchi kama Kenya na Mauritania, ziliuziwa kwa dola milioni 60 tu. Yote haya ni kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa ICSID [Tazama ICSID 41-2].
Ufisadi huu wa wazi wazi, uliopigiwa chepuo na wahafidhina wa rushwa nchini, ulimhuzunisha mno Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akasema: "Kama huu ndiyo ushirikiano wa nchi za Kusini [Malaysia na Tanzania], bora ukoloni urudi".
Ni kwamba, kufuatia jamii ya Kimataifa pamoja na Wafadhili kupaza sauti juu ya ufisadi huo, ilifikia mahali Rais [mpya] wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin Mkapa, kutaka kufuta Mradi huo, na kupongezwa kama hatua sahihi ya uwajibikaji kwa wananchi [East African alternative, September 1998, uk. 23].
Lakini katika mgeuko usiotarajiwa, Mkapa alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Malaysia, Mohamed Mahathir, wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Madola mjini Edinburgh, Aprili 1998; na kugeuzwa mawazo akakubali kwamba mradi huo ulikuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa nchi za Kusini [South – South Cooperation]; akafuta kusudio lake, japo alikwishabaini ufisadi huo kuweza kuhalalisha kufutwa kwa Mkataba. Na hilo ndilo alilopigia kelele Mwalimu.
Jumuiya ya Kimataifa yalonga
Na si Mwalimu tu aliyepiga kelele. Katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Tanzania na Wafadhili Jijini Dar Es Salaam, Desemba 6, 1997, [na tena Mei 2000], Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya [EU], Peter Christiansen, alieleza kusikitishwa kwake na Mkataba wa kifisadi wa IPTL, alisema: "Umoja wa Ulaya umesitushwa na kusikitishwa mno na ukimya wa Serikali ya Tanzania, juu ya jambo hili ambapo Viongozi wa juu wa Chama na Watendaji Waandamizi wa Serikali wanatajwa kuhusika na ufisadi katika mradi huu wa Kimalaysia – IPTL".
Akaendelea kusema: "Tunashindwa kuelewa nafasi na uhalali wa Mwanasheria Mkuu, na Waziri wa Madini na Nishati, kutia sahihi Mkataba wa IPTL [usiowahusu], ambao umeelezewa na Shirika la Fedha la Dunia [IMF] kuwa ni mzigo usiobebeka kwa uchumi wa nchi. …..Kashfa ya IPTL inazua maswali mengi kuliko majibu, jinsi kikundi kidogo cha wasomi, chenye kukosa uadilifu, kinaweza kuachwa kuendelea kunyonya wananchi masikini, kwa uchu na ulafi wa muda mfupi kwa kisingizio cha Ushirikiano wa nchi za Kusini …….Watanzania ni wanyonyaji wabaya kupindukia wa Watanzania".
Wananchi wa kawaida nao walishindwa kujizuia kulaani mradi huo wa kifisadi. Brigedia Jenerali Mstaafu, Joachim Burcard Ngonyani, alilalamika akisema, "Hebu tazama mkataba huu; ni mkataba wa kifisadi kwa viwango vyote. Tunataka wote waliouidhinisha washughulikiwe; uchu wao wa kujilimbikizia mali usiruhusiwe kudidimiza uchumi wa nchi hii" [The African, August 3, 1996]
Naye aliyekuwa Mbunge wa Dodoma Mjini, [hayati] Hashim Saggaf, alishangaa kuona waliotia sahihi mkataba huo walikuwa hawajakamatwa na kuhojiwa, waeleze kwa nini wametufikisha hapo [The East African, Aprili 26, 1999].
Uamuzi wa ICSID ulifurahiwa na Watanzania kama ushindi na ukombozi kwa TANESCO [Daily News 13/2/2001], wenye kunyoosha rekodi na maelezo, kwamba, biashara yoyote na IPTL lilikuwa janga kwa Taifa – kwa uchumi wa nchi na kwa mlaji, wakati kulikuwa vyanzo tele na rahisi, mbadala vya umeme nchini. [The East African 5/3/2001].
Hukumu yawachanganya IPTL
Hukumu ya ICSID haikutarajiwa wala kufurahiwa na vigogo watetezi wa IPTL serikalini ambao wakati kesi ikiendelea, walijitahidi kila wawezalo kuficha au kuharibu ushahidi, pamoja na kuwazuia mashahidi muhimu kwenda kutoa ushahidi kwa upande wa Serikali.
Rugemalila, kwa upande wake, alishituka baada ya kusoma ishara za mchezo na kutaka kuruka vihunzi asihusishwe na ufisadi wa IPTL, akaitupia mzigo Mechmar akisema, VIPEM kama mbia tu katika IPTL ilidanganywa na Mechmar juu ya gharama halisi za mradi, kama tu ambavyo TANESCO ilivyodanganywa na kampuni hiyo ya Malaysia.
Akaenda mbali zaidi kudai kuwa, Mei 9, 2001, alimwandikia Mshauri wa Fedha wa IPTL, Willy Lim, na aliyekuwa Waziri wa Madini na Nishati, Maokola Majogo, akitaka yeye [Rugemalila] asihusishwe na ufisadi huo; na akataka alipwe fidia na Mechmar ya dola 800,000, zikiwamo dola 200,000 kama gharama alizoingia kati ya 1994 – 2001; na dola 80,000 gharama za kusafiri kwenda London na Kuala Lumpar; na fidia ya ardhi na gharama za Kisheria, dola 350,000.
Katika barua pepe ya Juni 2001, Willy Lim alimkandia Rugemalila akimlaumu kumwandikia Waziri Majogo akihoji: "Ulikuwa ukifikiri nini kwa kuandika hivyo? Kwamba wewe hustahili kulaumiwa……? Kwamba kwa fikira zako unalinganisha "kudanganywa" kwako na Mechmar kuwa sawa na jinsi TANESCO "ilivyodanganywa" na Mechmar? Huwezi kusema bila kuinamisha kichwa kwa aibu, kwamba unayo matakwa na mapenzi kwa IPTL moyoni mwako".
Ikichukuliwa kwamba Rugemalila ndiye aliyekuwa kiunganishi [a – go between] mkubwa kati ya IPTL na vigogo wa BOT pamoja na taasisi za umma tangu mwaka 1994 katika Mradi huu; huwezi kushindwa kuamini kwamba, Washirika hawa wawili [IPTL na Rugemalila] katika mradi huu tata, walianza kurukana baada ya "kufumaniwa".
Katika hatua nyingine ya kutaka kuchanja mbuga, Februari 2, 2002, mwezi mmoja tu tangu umeme wa IPTL kuingizwa kwenye gridi ya Taifa, Rugemalila [VIPEM] alifungua shauri Mahakama Kuu kutaka kuvunjwa kwa IPTL, ila tu kama angelipwa asilimia 30 ya thamani ya mali za kampuni hilo. Na shauri hili [Misc. Civil Cause No. 49 of 2002] ni mojawapo ya Kesi mbili zilizotolewa uamuzi kwa pamoja na Jaji Utamwa hivi karibuni [kama Consolidated Misc. Cause No. 49 of 2002 and 254 of 2003], kama tutakavyoona hivi punde.
VIPEM walifikia hatua hiyo mwaka 2002, baada ya kubaini wasingeweza kupata mgawo stahili, waliokadiria kuwa dola milioni 100, katika mkataba huo wa miaka 20 na Mechmar; wakaanza mazungumzo na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii [NSSF] ili kuliuzia hisa hizo kwa kiwango hicho. Hii ilihitaji kuteuliwa kwa Mfilisi [Liquidator] wa Kampuni ya IPTL ili kusimamia mali na masuala mengineyo yanayohusu ubia huo.
Nini kilitokea? Na hiki kinachoitwa fedha za Akaunti ya "Escrow" ya IPTL, inayodaiwa kuchotwa zaidi ya Shilingi bilioni 200/= katika mazingira tatanishi, na kuzua mtetemo na ghadhabu bungeni na kwa jamii, ni kitu gani?
Chanzo: Raia Mwema ya 13 Aug 2014