Ipp media na sahara media - joint venture basic transmission

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,198
Reaction score
11,631
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma, (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, (wa 2 kushoto) leseni ya kujenga

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra), imeipa kampuni ya Basic Transmission, leseni inayoiruhusu kujenga miundombinu ya mawasiliano yanayotumia mfumo wa kisasa wa digitali.

Kwa kupewa leseni hiyo, vituo vya redio na televisheni za biashara, vitakuwa vinapeleka matangazo kwa kampuni hiyo ili yasambazwe nchi nzima.
Kampuni ya Basic Transmission inamilikiwa kwa ushirikiano wa IPP Limited na Sahara Communications.
Ilikabidhiwa leseni hiyo jana katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Tcra jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Reginald Mengi, alipokea leseni iliyotolewa na Tcra kwa niaba ya kampuni hiyo.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Sahara Communications, Samwel Nyala.
Mkurugenzi Mkuu wa Tcra, Profesa John Nkoma, alisema mbali na kujenga mtandao wa mawasiliano, kampuni hiyo ina haki ya kuendesha mawasiliano ya simu.
"Leseni hii ni sawa na ile waliyopewa Vodacom," alisema Profesa Nkoma.
Akipokea leseni hiyo, Mengi aliisifu Tcra kuwa ni shirika la umma lenye kutoa ushirikiano bila masharti, na hivyo kufuta hisia mbaya za kujihusisha na `mchezo mchafu’ ili kuwasafishia njia baadhi ya watu.
"Tanzania mara nyingi tunapozungumzia mashirika ya umma, kuna hisia kwamba unaposhirikiana na mashirika haya unatakiwa utoe chochote ujisafishie njia,” alisema.
Aliongeza: “lakini wote tukiulizwa ni shirika gani, ambalo linatoa ushirikiano bila kutoa chochote, jibu utapata ni Tcra kwa sababu ni shirika linalotoa haki sawa kwa watu wote."
Alisema mbali na hayo, Tcra pia imekuwa ni mtandao wa kwanza barani Afrika kushughulikia muingiliano wa mawasiliano.
Mengi aliishukuru Tcra kwa kutambua kuwa uwezo wa kampuni hiyo kujenga mtandao wa mawasiliano nchini, yanayotumia mfumo wa kisasa wa digitali.
Katika hafla hiyo, Tcra ilitoa leseni ya utangazaji kwa vituo vinne vya redio. Vituo hivyo na mikoa vinakopatikana kwenye mabano, ni Hot FM (Iringa), Generation FM (Mbeya), Baraka FM (Mtwara) na Pride FM.
SOURCE: NIPASHE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…