abudist
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 850
- 781
Leo hii tuna kauli za viongozi wawili wote wa serikali kuhusu swala moja linalohusu shutuma za mkuu wa mkoa wa Dar kuivamia studio ya Clouds kwa mitutu.
Sasa Mh. Nape Nnauye kwa madaraka ya serikali aliyonayo kama waziri wa wizara husika ameunda tume ya uchunguzi. Jambo ambalo ni zuri na amehahidi matokeo yatakuwa ya uwazi na hatua stahiki zitachukuliwa. Amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba 'Sisi serikali tunawapa pole Clouds kwa kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa sababu kajiridhisha kilichotokea' Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati anaongea kwenye uzinduzi wa barabara (Fly Over), Amesema yeye ni rais wa waTanzania wote na maendeleo hayana chama na ndiyo maana (Fly Over) zinajengwa kwenye jimbo la Chadema. Kitu ambacho ni kweli. Sasa Rais yeye ni serikali pia, na ndiyo muuongozaji wa serikali. Kwa rais anataka mawaziri wachape kazi pamoja na viongozi wake wote. Mh. Nape bila kigugumizi kachapa kazi yake sawasawa bila kuchelewa. Kwa maana hiyo hata Rais lazima amsifu kwa hilo. Huyu sio waziri siyo mzigo na ndiye namna ya waziri anayetakiwa na Rais Magufuli.
Wakati huo huo kwenye hotuba hiyo ya Rais ameshindwa yeye kama kiongozi wa serikali kuwapa pole Clouds kwa kile kilichotokea. Lakini ameendelea kusisitiza kwamba mkuu wa mkoa Daudi Bashite a.k.a Paul Makonda aendelee kufanya kazi. Sasa ina maana Mh Rais hapo kwanza anakubaliana na kitendo cha Makonda dhidi ya Clouds kama sahihi. Si ndiyo? Sababu anamhamasisha aendelee na kutumia madaraka vibaya. Kwa hiyo ina maana rais anamaanisha chochote anachofanya Makonda ni sawa tu hata kama kama cha kuvunja sheria ilimradi yeye na Makonda wameridhia. Sasa hii tume ya halali Mh. Nape aliyoituma kufanya kazi faida yake nini? Wakati haina baraka ya Rais na ameshaihukumu tayari? Hapo tuna kauli mbili tayari za kutoka kwenye serikali moja ambazo zinapingana.
1) Kauli moja ya kwanza ya busara na utaratibu. Kwamba tume imeundwa ili tujue lipi limetokea na hatua stahiki zichukuliwe
2) Kauli ya pili ya kibabe kwamba, mimi ndiye Rais ninachofanya chochote hakuna mtu wa kukipinga wala kutoa maamuzi mengine hata kama ya kisheria.
Nchi hii inaelekea wapi? Hapa demokrasia na utawala bora unaanza kupotea. Kama kiongozi mmoja anaweza kuchukua jeshi lenye silaha kwenda kutisha taasisi kwenye shughuli zao. Tena siyo kawa shughuli za maendeleo bali kwa matakwa binafsi yasiyo halali. Na kibaya zaidi kiongozi huyu wala hakutakiwa kuwa kwenye wadhifa huo kutokana na tuhuma za vyeti zinazomkabili.