Ipi bora? Kuingia Mkataba (Uber) au Kupeleka Hesabu (Daladala?)

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
828
Naanza na salamu kwa Wakubwa, bila kuwasahau Wadogo.

Nilishakuja hapa JF kuomba ushauri kutaka kuahirisha chuo kwa kijana wangu baada ya (mimi) kukwama kiuchumi ili aje mtaani tupambane na mwaka unaofuata akaombe kuendelea na Bachelor yake. ( ninawashukuru wote waliochangia hoja.)

Katika pitapita zangu nimepelekwa kwa wafadhili niliwapa hoja yangu kwanini nimewafuata, wapo walioguswa na kuahidi kutoa ufadhili aidha uwe wa Mali au Hali.

Kilichonileta kwenu wana JF nikuomba ushauri utakaokidhi matakwa yangu. Mmoja wa hao wafadhili kaniambia nitafute washauri ambao watanishauri, anunue gari dogo ili tuingie nae Mkataba kwa ajili ya kufanyabiashara ya Taxi mtandao, au niendesha Daladala na kupeleka Hesabu.
 
Kiufupi tu biashara ya daladala ina uhakika wa kulala na hela.
Hiyo ya uber ni kubahatisha tu leo unapata kesho hupati.
Mimi sio dereva ila nawaona wanaoendesha daladala wana uhakika wa maisha kuliko hao wengine.
 
Yaani hapo umepewa uchague kati ya range rover na bajaj afu unaomba ushauri?

Bila hata kujiuliza chukua hio daladala fasta
 
Back
Top Bottom