Kwa yeyote ambaye anakusudia kununua simu aina ya iPhone na ambayo imeshatumika, ikiwa kwa mtu au dukani anatakiwa ahakikishe ya kuwa :
Simu hiyo iko wazi yaani haihitaji pass code au Apple ID.
Pia ili kuhakikisha kama haijawekwa passcode itabidi uizime na kuiwasha mara mbili tatu ili uridhike.
Ama kuhakikisha kama simu haina apple id kwanza itabidi ujiunge na internet ndipo utaweza kujua.
La kufanya jiunge na internet, kama kwa Wi Fi au njia nyengine, kisha nenda kwenye Apple Store.
Ukifika hapo binya Search, hapo sehemu ya juu ya Search andika neno 'jamii forums'. Chagua 'jamiiforums' kisha bonyeza FREE kisha inakuja INSTAL.
Kama umekusudia kuINSTAL hapo ndipo utatakiwa kuweka apple id, na ikiwa hakutakiwi kuweka apple id inamaanisha ya kuwa simu iko wazi.
Kisha jaribu kuINSTAL kitu chengine ili uzidi kuhakikisha ya kuwa unauziwa kitu chenye dhamana.
Ushauri wangu ni bora mtu ukubali kusumbuka japo kidogo ili mradi wako uwe kuliko kuuziwa kitu ambacho huna uhakika nacho. 🌺