Kama ni mfanyabiashara mdogo (micro) siyo lazima uwe na hivyo vitu kwa gharama kubwa. Vipo ambavyo vimeishachapishwa tayari. Wewe unanunua na kubandika mhuri wenye jina la biashara yako pamoja na taarifa zingine kama namba ya mlipa kodi (TIN), sanduku la posta, n.k. Hizo unaweza kuzipata kwenye maduka makubwa ya stationery kama Masumin au hata pale Game (Mlimani City).