Msaada juu ya upatikanaji wa satellite internet dish kwa matumizi ya internet kwa Tanzania hii ni sehemu gan naweza nunua. Na gharama yakr je? Msaada kama kuna mtu anayejua anipe mwongozo kuanzia gharama
Gharama kubwa na speed ya kobe, na hata speed ikiwa kubwa basi ping ni majanga. Tumia satelite internet mahala ambapo internet ya simu haipatikani kabisa.
Unanunua dish tokana na provider wako. Kuna madish mengi kama
-Ka band
-ku band ambalo muonekano wake ni kama wa dish la azam
-C band ambalo ni kama yale madish ya zamani makubwa.
Kuna jamaa wanajiita quika walipromise internet ya bure ya satelite ila naona kama ni danganya toto, nimejaribu mara kibao kuwasiliana nao bila mafanikio, nilitaka kuitest nione.
Wacheki Blink , speed ya kuridhisha sana. angalia attached pic kuona plan zao baada ya installation, ila installation itakucost around $500 au zaidi.
PS: Ninawatumia personally na sehemu ni very remote ambapo hakuna internet coverage ya telecom companies au ni 2g tu ndo inashika(zaidi ya moja). so nina experience ya ninacho suggest, ingawa ni expensive.