JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Katika miaka ya karibuni, kuzimwa kwa intaneti wakati wa uchaguzi kumegeuka kuwa jambo la kawaida katika baadhi ya nchi za Afrika. Mataifa kama Tanzania na Uganda yameshuhudia kufungwa kwa mitandao ya kijamii au kuzimwa kabisa kwa huduma za intaneti kipindi ambacho wananchi wanahitaji taarifa zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Hali hii imeibua mjadala mpana kuhusu hatma ya demokrasia na haki za msingi za wananchi.
Mifano ipo wazi. Uganda ilizima intaneti na mitandao ya kijamii wakati wa uchaguzi wa mwaka 2021 na imefanya hivyo 2026, ikidai sababu za kiusalama. Tanzania, katika chaguzi zilizopita, ilishuhudia upatikanaji mdogo au kufungwa kwa majukwaa kama X (Twitter) na WhatsApp JamiiForums, uchaguzi Mkuu 2025 internet ilizimwa kabisa, hali iliyodhibiti kwa kiasi kikubwa mawasiliano ya wananchi.
Ethiopia pia imekuwa ikizima intaneti mara kwa mara, si tu wakati wa uchaguzi bali pia wakati wa migogoro ya kisiasa, hali iliyonyima mamilioni ya watu taarifa muhimu.Nchi nyingine kama Sudan, Guinea, Chad na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimewahi kutumia mbinu kama hiyo.
Kinachofanana katika mifano hii ni hofu ya taarifa huru na uwezo wa wananchi kufuatilia na kuripoti mwenendo wa uchaguzi kwa wakati halisi. Badala ya kuzima uvumi, hatua hizi mara nyingi huongeza sintofahamu na kuimarisha hisia za kutokuaminiana kati ya serikali na wananchi.
Kuzima intaneti kunakiuka haki ya msingi ya kupata na kusambaza taarifa. Katika zama za kidijitali, intaneti si anasa bali ni miundombinu muhimu ya kiraia, sawa na barabara au umeme. Kuizima ni sawa na kuzima sauti za wananchi wakati zinapohitajika zaidi.
Intaneti si tishio kwa demokrasia, bali ni kioo kinachoonesha uhalisia wa uongozi. Changamoto kubwa ni uelewa duni wa thamani ya uwazi na uwajibikaji. Badala ya kuzima intaneti, serikali zinapaswa kujenga mifumo imara ya uchaguzi inayokubali uhakiki na ukosoaji wa wazi kama nguzo ya demokrasia ya kweli.