dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Mkongwe katika muziki wa Hip Hop Bongo, Inspector ‘Babu’ Haroon, amesema anamshukuru Mungu kwa kumjaalia kukamilisha ujenzi wa nyumba zake mbili jijini Dar es salaam.
Akizungumza kupitia Segment ya ‘Nje Ndani’ inayoruka kupitia Times Fm, Hit maker huyo wa ‘Asali ya moyo’ alidai watu wengi hawajui kama yeye amevuna pesa kadhaa za kumtosha kiasi tangu aanze muziki.
“Mpaka sasa hivi kuna sehemu kama mbili zimeshakamilika kabisa, nyumba mbili, ya kwanza ipo Kongowe na nyingine ukivuka kivule panaitwa Ngondole” Alifunguka.
Katika hatua nyingine msanii huyo alidai hababaishwi na baadhi ya wasanii wenzake wa Hip Hop wanaomuimba vibaya kwenye Lines zao, kwa sababu wanamtumia kama daraja la kuyafikia mafanikio.