jikuTech
JF-Expert Member
- Apr 9, 2023
- 228
- 290
COMPILER NI NINI ??
Kwa lugha rahisi , compiler ni kama mtafsiri ambaye hubadilisha maelezo yaliyoandikwa katika lugha za programu ambazo sisi binadamu tunaelewa kam vile python, java, C++ na kubadilisha maelezo hayo kuwa lugha ambayo lugha inaweza kuelewa moja kwa moja (mashine language) ambayo ni mfululizo wa nambari mbili (0 na 1).Mfano rahisi Fikiria unapoandika maandishi katika llugha ya kiingereza . ili mtu anayezungumza kifaransa aweze kufuatilia maandishi hayo unahitaji mtafsri abadili maandishi hayo kuwa kifaransa.
Hivyo hivyo compiler inachukua code za programu zinazo andikwa kwa lugha ya programu flani na kubadilisha code hizo kuwa mashine code ambazo kompyuta inaweza kutekeleza.
Kwa nini sasa tunahitaji compiler?
Tuna hitaji hii kitu kwa kuwa compyuta hazielewi lugha zetu na ikiwa zinaweza kompyuta kufanya mahesabu kwa haraka sana lakini tatizo hazielewi lugha za programu kama python , java n.k na ndio maana compiler ikawepo.
Mchakato wa Compilation
- Unaandika maelezo ya programu yako kwa kutumia lugha ya programu unayoipenda, hizi huitwa code za mwanzo .
- Compiler inasoma code zako za mwanzo na kuzikagua ili kuona kama kuna makosa gani ya kiuandishi , kiutaratibu au kwa lugha ya programming inaitwa syntax
- Ikiwa hakuna makosa compile hubadilisha code za mwanzo na kuwa machine code
- Mashine code huhifadhiwa kama faili ambalo kompyuta inaweza kuliendesha moja kwa moja. View 12