Information Technology(IT-TEHAMA)-04

Information Technology(IT-TEHAMA)-04

jikuTech

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2023
Posts
228
Reaction score
290

UMUHIMU WA KOMPYUTA SKILLS​

Katika kipindi hiki cha kidigitali, Ujuzi wa Kompyuta umekuwa ni muhimu sana ili kufanikiwa katika majukumu yaliyopo katika maeneo mbalimbali maishani. Maeneo hayo hususani kielimu, kazini na mambo binafsi

Kompyuta na vifaa mbalimbali vya umeme vimeleta mapinduzi ya namna tunavyo takiwa kuishi , namna tunavyo weza kufanya kazi, namna tunavyoweza kutafuta taarifa , namna tunavyo weza kuwasiliana na wengine na namna tunavyo weza kufanikisha shughuli zetu kiurahisi na kwa ufanisi mkubwa

Hizi ni baadhi ya sababu za kwa nini ujuzi wa komputer ni muhimu katika kipindi hiki cha kidijitali ??

UFANISI: Kwa kutumia Kompyuta unaweza fanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi (yaani haraka na bila kukosea) kwa mfano unaweza tumia Kompyuta kuandaa nyaraka , kutuma barua pepe na kufanya utafuta wa taarifa za kitafiti mbalimbali kwa njia ya mtandao (online search) huu ujuzi utakusaidia kurahisha utendaji na kuongeza uwezo wako kwa kuokoa muda
MAWASILIANO: Kompyuta na vifaa vya kidijitali vimerahisisha namna ya kufanya mawasiliano kwa urahisi. Kwa kutumia ujuzi wa Kompyuta unaweza wasiliana na mtu kupitia Email, mikutano ya video, Mitandao ya kijamii, na majukwa mbalimbali ya mtandaoni duniani kote.

MAENDELEO YA KAZI: Fursa mbalimbali za kazi siku hizi zinahitaji sana kuajili mtendaji ambaye angalau anakuwa na ujuzi wa Kompyuta. Kwa kuwa ujuzi wa Kompyuta unampa mtu uwezo wa kutumia Program mbalimbali za Kompyuta, Uwezo wa kufanya utafiti na Na ujuzi au uwezo wa kupangilia taarifa mbalimbali na kuzichakata kwa ufanisi. Kwa hivyo katika kipengele hiki uwezo mzuri wa kutumia Kompyuta unaweza kukutofautisha na wengine katika fursa flani .

UTAFUTAJI WA TAARIFA: Ujuzi wa Kompyuta una mpa mtu uwezo wa kutafuta taarifa rasmi mbalimbali rasmi katika mtandao. (Internet) kwa kutumia search engine (engine za utafutaji) mtu unaweza tafuta taarifa yoyote kuhusiana na jambo lolote mtandaoni mahali popote pale duniani.

UBUNIFU: Kwa kutumia ujuzi wa Kompyuta mtu anaweza fanya jambo lolote la kibunifu kwa kutumia Kompyuta yake kwa namna anavyo taka. Mfano mtu anaweza fanya uzalishaji wa video anaweza tengeneza mitindo mbalimbali ya kibunifu (graphics designing), uzalishaji wa muziki. View 05

Bonyeza HAPA Ingia kwenye mafunzo haya, Ujifunze moja kwa moja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom