mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 343
- 359
Tafsiri kutoka gazeti la The Hindu
INDIA imelaani vikali Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislam(OIC),ikisema kuwa Jumuiya hiyo imepoteza uaminifu kufuatia ziara ya Katibu Mkuu wake Hissein Brahim Taha, Katika Mpaka wa Pamoja wa India na Pakistan
Taha alikuwa katika ziara ya siku tatu iliyoanza Desemba 10 katika mpaka huo kwenye eneo la Kashmir inayokaliwa na Pakistan.
Maoni hayo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya India yalikuja baada ya Katibu Mkuu wa OIC Hissein Brahim Taha kutembelea eneo la uthibiti wa Pamoja na akiwa katika upande wa Pakistani na kujulishwa hali na jeshi la Pakistani.
Bwana Taha pia aliomba dua na kukutana na watu wanaodaiwa kuathiriwa na Makombora kutoka Upande wa India.
Akitoa msimamo rasmi wa serikali juu ya ziara hiyo ya Taha,Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje wa India Arindam Bagchi,alisema
“Wacha nirudie Kwamba OIC haina Msimamo katika masuala yanayohusiana na J&K,ambayo ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya India
"Jaribio lolote la kuingilia masuala ya ndani ya India linalofanywa na OIC kupitia Katibu Mkuu wake halikubaliki kabisa”alisema Arindam Bagchi.
Bagchi aliongeza kusema kuwa Katibu Mkuu wa OIC amekuwa ‘msemaji’ wa Pakistani na kwamba Jumuiya hiyo limekuwa likichukua Mtazamo wa Kijumuiya kwa Upendeleo na Ukweli usio sahihi wa masuala .
“Tunatumai kwamba angejiepusha na kuwa mshirika katika kutekeleza ajenda chafu ya Pakistani ya kukuza Ugaidi wa Mipaka hadi India haswa katika J&K”alisema Msemaji huyo wa India.
Hapo awali bwana Taha,ambaye anatoka Chad,alikutana na Uongozi wa Pakistani akiwemo Waziri Mkuu Shebhaz Sharif.