India kuna matabaka tena makubwa ya wao kwa wao, na tabaka linalodharauliwa zaidi na ambali ni maskini zaidi ni kutoka South India. South India ndipo wanapopatikana wahindi weusi, ndio maskini sana kule sub continent ya India. Miji ya Mumbai, Delhi Amritsar, Hyderabadi kuna ubaguzi sana ambapo huwezi kwenda kutembea kwenye maeneo ya wakubwa na utajishtukia kama si kutemwa mate.
Kwenye miji kama Gujarat na sehemu zingine kama Qadian, kule walau kuna usawa zaidi maana kuna muingiliano wa dini kidogo na imesaidia maana utakuta waislam na wakristo wanapatikana.
Ukiwakuta wahindi wenyewe ambao ni Hindu wanaoabudu kwenye srinigar, au wale wenye imani ya masingasinga...huko ni 100% ubaguzi.
Kutokana na over population ya India, toka mwanzoni mwa miaka ya 1900 wahindi wengi walihama kwao na kukimbilia nchi za Afrika ambapo walizaliana, wakapata watoto, wakapata wajukuu na wamesalia kuwa ni raia halisi tena kwa kuzaliwa. Kitu ambacho sisi waafrika hatukuweza kulikimbia bara hili na kwenda kutafuta makazi/maisha kwao India. Ndio maana mpaka leo hii, tunao viongozi ambao wana asili ya India kama vile Prof Issa Shivji etc.
Kaka umeeleza vizuri ila nikurekebishe hapo uliposema South India ndio wanaongoza kwa umaskini,SI KWELI,mimi nipo Bangalore(IT city of India) na moja ya miji inayokua kwa kasi India,miji mingine ya South ni Chennai(Industrial Hub of India due to large port),hydrebad na Kerala(state with largest educated people who scattered all over the world),na hapa Bangalore ni moja ya majiji yenye wageni wengi sana hususan wa Africa wanaokuja kusoma,pia wahindi wengine wanaotoka North(hususani Chinks....wanaofanana na wachina wanatokea Assam,Sikim n.k).
Pia ukiangalia states kama Jarkhandi,Bihar,Rajahstan na Sikkim,ni maskin sana.
Uzuri wa huku kusini ubaguzi si mkubwa sana sababu zikiwa ni pamoja na kuwepo kwa wakristu,waislam wengi pia elimu imewasaidia maana watu wamepata exposure kama ya kwenda US,UK,Dubai na sababu kubwa ni IT companies kama INFOSYS na WIPRO ambazo headquarters zao zipo hapa Bangalore.
Ila pia sio siri ubaguzi bado upo,mfano mim mwenyewe nina rafiki yangu msichana,tukiwa tunaongozana barabarani utaona vijana wanatukana au wanamkashifu huyo dada.
Pia kwaupande mwingine sisi wenyewe waafrika tunachangia unakuta watu wana fanya after parties mpaka saa nane za usiku wakibughuzi watu waliolala,wasichana wanavaa nusu uchi kabisa ambapo huko nyumbani wasingethubutu,pia watu kama wanigeria wanajihusisha na biashara harama kama kuiba kwa kutumia debit cards,drugs n,k.