Inawezekana sasa Lowasa ni saizi ya Mbowe

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,311
3,341
Ni ukweli usiopinginga kwa muda mrefu Mbowe hakua na saizi yake ndani ya CDM na hili alililinda kwa nguvu na mbinu zake zote kuhakikisha hakuna mwenye japo kuikaribia saizi yake.
Viashiria vinaonesha kwamba wote waliojaribu kuikaribia nafasi yake kwa kujifanya saizi yake ama kwa kumpinga ama kua na mtizamo tofauti na wake waliishia pabaya na mifano ni mingi sana kuthibitisha hili.
Tetesi zilizagaa alihakikisha anakua na mtandao wakulinda na kutetea maslah yake kwa kila namna ikibidi wale hatarishi wote kutolewa kafara eidha kwakutimuliwa ama kupewa makalipio makali.
Tunafahamu kilichowapata ZZK na kundi lake tulitetesiwa wakati ule kwamba chanzo kilikua ni kujaribu kukisogelea kiti cha enzi jambo ambalo hatima yake waliitwa wasaliti na hatimaye kutimuliwa chamani.Nisisitize kwamba tulitetesiwa lakini viashiria vilionesha kuna ukweli kwenye lile lililo semwa.
Ni ukweli wa wazi Mh Mbowe anamafanikio makubwa ndani ya CDM na ni dhahiri huwezi kutaja mafanikio ya CDM ya sasa usimtaje Mbowe na kimsingi kutokumpa sifa hii litakua ni kosa kubwa kwani ni sifa anayoistahili kwa mengi mazuri aliyoyafanya CDM.
Licha ya mazuri haya ya mh Mbowe bado haimaanishi kwamba hakuna kama Mbowe na hatotokea kama yeye tena.
Lakini sasa kuna viashiria vyote mh Lowasa amekua si tu saizi ya mbowe ila huenda akawa hata zaidi ya yeyote chamani jambo ambalo hapo mwazo lilikua gumu kutokea.
Sasa tunaona mh Lowasa anadiriki hata kukosoa mtizamo wa Mwenyekiti ambeye hapo mwanzo alikua ni untouchable.
"Chama kina process,Chadema sasa tumesha graduate tulisha vuka kwenye uanaharakati hatuhitaji maandamano tena".Hii ni kauli ya Lowasa na tunaona mara tu kauli hii ilipotolewa tunamuona Mbowe anatoka kwenye vyombo vya habari kuwataka BAVICHA wasiende dodoma kuendeleza harakati zakuzuia mkutano wa CCM.
Hivi ni nani aliweza kumkosoa hapo nyuma na akabaki salama?
Kwa hakika Lowasa si tu saizi ya Mbowe bali huwenda ni zaidi ya yeyote chamani.
 
Mbowe atabaki kuwa yeye na Lowassa atabaki kuwa yeye .
Sisi hatuangalii mtu tunaangalia maendeleo ya chama.
 
Kwahiyo kwasasa sio fisadi tena ila ni kiboko ya mwenyekiti? Yaani kama umezidiwa uwezo wa kupambanua mambo na Sendeka basi wewe ni bure kabisa.
 
Jamani wana ccm tumewachoka kila kukicha Lowassa Lowassa hamchoki? Simmesema tuwaache mjenge Nchi? Mbona asubuhi Lowassa , mchana Lowassa mwacheni Na Chadema yake
 
Jamani wana ccm tumewachoka kila kukicha Lowassa Lowassa hamchoki? Simmesema tuwaache mjenge Nchi? Mbona asubuhi Lowassa , mchana Lowassa mwacheni Na Chadema yake
Tunawasaidia kuyasemea mapungufu ya mwenyekiti wenu ninyi hamna ubavu wakuyasemea mnaogopa kutimuliwa
 
Back
Top Bottom