Inasikitisha, Vijana wanaobeba makapu ya Rangi kupaka wadada

Good Man

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
931
1,159
NAMI NALISAKA KAPU, NIPAKE KUCHA WADADA – 03/01/2015

Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada
Ni kama vile upupu, hii kazi ya faida
Siwezi toka patupu, najua zake faida
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Hebu pita pale Mwenge, uone vyake vioja
Mambo mengine use***, waosha hata mapaja
Sio tuu pale Mwenge, kwingine siwezi taja
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Wapaka rangi vidole, mikono na miguuni
Hakuna cha kwenda shule, ufundi wa mtaani
Sio John wala Sele, wote wapo kwenye fani
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Mguu wa Yule dada, alaza kwa Yule kaka
Dada haioni shida, mwenyewe afarijika
Amuosha Yule dada, upenuni anafika
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Upaja automasa, eti kisa amuosha
Haya mambo ya kisasa, kwa kweli yahuzunisha
Yanabaki yatutesa, wao yawafurahisha
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Wengine na majumbani, wapaka wake za watu
Leo yupo sebuleni, afanya yake mavitu
Kesho hadi kitandani, hapo tena kila kitu
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Hivi kuosha mguu, wenyewe ni hawawezi?
Ninabaki mimi duu, Nabaki mdomo wazi
Wapo waoshwa miguu, walala na usingizi
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Mtaji ni lao kapu, na virangi rangi Fulani
Kazi hutoki patupu, wapata vitu Fulani
Utakunywa hata supu, kama si mambo Fulani
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Naingia mzigoni, nipate kuosha watu
Hata haya siioni, siangalii ya watu
Kapu langu mkononi, naita dada za watu
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Yeyote akijirengesha, kumuacha sitaraji
Haya yote ni maisha, naanza saka mtaji
Miguu kwani kuosha, elimu haihitaji
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

Yule mke wangu mimi, hapakwi rangi na mtu
Dhihaka wala sisemi, nitaja kuua mtu
Ni bora na kujihami, asije kuliwa vitu
Nami nalisaka kapu, nipake kucha wadada

MSAFIRI M. ZOMBE
MWANA WA KIGAMBONI
 
Hii kazi nzuri ila inachosha haraka....mimi niliachana nayo miaka kama 10 iliyopita na kujikita kwenye kuuza maji hapa mjini baada ya kugundua kuwa wadada na kina mama wengi hapa mjini wanapenda kuogeshwa na kusuguliwa mgongoni. Toka nianze hii kazi ya kuuza maji, kwa kweli sina tena hamu ya kuoa.
 
JUDGE 1;
Utunzi mzuri lakini ungejitahidi kujaza nyama na utamu hizo beti zako ikiwemo kupachika vijichekesho other wise you've done well..

JUDGE 2;
Pia unge zingatia lugha ya picha, na kutia punch line nzito nzito zenye ku amsha ,hisia na kumhamisha msomaji ki fikra..nice work

JUDGE 3;
unajua ngoja nikushauri kitu kimoja badala ya kutumia neno "nikapake" ungetumia kimalizio kama "NAMI NALISAKA KAPU NIKACHORE KUCHA WADADA" Otherwise utunzi wako ume simamia ukucha..
 
Hii kazi nzuri ila inachosha haraka....mimi niliachana nayo miaka kama 10 iliyopita na kujikita kwenye kuuza maji hapa mjini baada ya kugundua kuwa wadada na kina mama wengi hapa mjini wanapenda kuogeshwa na kusuguliwa mgongoni. Toka nianze hii kazi ya kuuza maji, kwa kweli sina tena hamu ya kuoa.
Duh mkuu hii unaifanyia maeneo gani maana hili ni jipu kubwa
 
Back
Top Bottom