Ina maana watanzania na serikali tumeshindwa kuzuia mambo haya

dogo_mjuaji

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
222
48
habari wanajamvi
Kumekuwa na tabia inayonishangaza sana hasa maeneo ya mjini ambapo utakuta mtu anayejiita daktari wa tiba asilia akidanganya wananchi wengine kuwa anatoa tiba na mara nyingi utakuta amekusanya watu katikati ya barabara mfano hii msimbaz road na uhuru road mpaka maeneo ya buguruni huku akijitapa kuwa anatibu nguvu za kiume na tiba hizo mbadala zinakuwa hazijathibitishwa.
Au pia kuna wale matapeli wengine wanaokaa pembezon mwa barabarara na kurushia wapita njia vitu ambavyo mwisho wa siku wanakuja kutapeli(inaniuma sana nikikumbuka nlivotapeliwa 5000 kwenye ule mchezo wa karata 3)
Anyway siwezi kumpangia homo sapiens mwenzangu namna ya kuishi akienda kucheza au kuwasikiliza watu hawa basi kapenda mwenyewe lakini je watu hawa wapo kihalali?
Sasa hoja yangu hapa ni kuwa ina maana hata wananchi wameshindwa kuwafukuza matapeli wa aina hizo hapo juu ilihali wanazuia njia kwa kufanya shughuli zao zinazosababisha msongamano na kero hasa kwa sauti zao?
Au vitu vingne mpaka serikali hii sikivu iviingilie kati?
ivi kweli kitendo cha kuwatimua hawa matapeli nacho tunaona aibu?
ebu tuweni serious kwa kweli
Wale wanaotuibia mabilioni wametuzidi ujanja hatuwezi wafanya kitu hadi hawa wadogowadogo nako tunawashindwa?
 
Back
Top Bottom