In anger there is no intelligence.

In anger there is no intelligence.

DSN

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
2,837
Reaction score
1,686
Kuhusu sakata la Richmond, ambalo lilimfanya ajiuzulu uwaziri mkuu, Lowassa alisema tatizo kubwa halikuwa kuhusu mitambo hiyo ya umeme ila uwaziri mkuu. "Ajenda haikuwa kuhusu Richmond, ila uwaziri mkuu ndiyo maana niliwaachia.
Anger against people known to him, unknown to Public.

Lakini jingine tulilojifunza katika ubishi ule umeisababisha nchi hasara ya Dola 120 milioni,"
Anger created to the Public by him.

"Moja ya ushauri wangu wakati ule ilikuwa ni kutaka kuvunja mkataba wa Richmond nikaita wataalamu, nikawaelezea kuhusu habari za magazeti kuwa zinasema hawa jamaa (Richmond) hawana fedha, hebu angalieni, nikaita wataalamu na mwanasheria mkuu, nikawaambia kuna hii habari kuweni makini, pamoja na hayo nikaweka kwa maandishi kwa mwanasheria mkuu, pia kulikuwa na timu ya mashauriano ya Serikali iliyokuwa chini ya makatibu wakuu nao walikuwa na vikao vyao, ilikuwa inaongozwa na (Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Gray Mgonja) nao wakakutana chini ya Katibu Mkuu Kiongozi na baada ya kukutana wakatoa uamuzi ambao sina haja ya kuujadili. Lakini ubishi ule umetugharimu Dola 120 milioni.
"Nilipotaka mkataba uvunjwe nilikuwa nimetoa uzoefu wangu kwani kabla ya kuwa waziri mkuu nilikuwa nimekuwa waziri wa maji na mifugo ambako nilivunja mkataba wa kampuni ya Kiingereza iliyokuwa imewekeza katika mradi wa maji Dar es Salaam ya City Water.
Hidden anger Against The Cabinet Of United Republic Of Tanzania.

Naamini kuwa kama tungeanza kwa kasi ile tuliyoanza nayo nikiwa waziri mkuu, sasa ningepita napunga mkono ningepata kura zote…
Hidden anger against unfullfilled interest...
lakini kinachonisikitisha tumekuwa hatufanyi maamuzi magumu au rahisi, kila kitu kinakwenda legelege.
Anger of wishes

Akizungumzia kuhusu kupingana na kaulimbiu ya Serikali ya ‘Kilimo Kwanza', Lowassa alisema ataendelea kushikilia msimamo huo kwa sababu elimu ndiyo kila kitu katika maisha ya mwanadamu. "Mimi sikubaliani na wenzangu wanajua, sikubaliani na kilimo kwanza, naamini ‘elimu kabla, kilimo kwanza baadaye'.
Anger to go agaisnt his mates.

]"Wakati ule nilisema hilo, waziri mmoja akanishambulia akinipinga akisema takwimu zangu si sahihi na hakuna tatizo, lakini bado mimi naamini kuna tatizo kubwa.
Anger when he is challenged, being out of Power.

]"Alipotakiwa kuzungumzia uhusiano wake na Rais Jakaya Kikwete, Lowassa alisema hadhani kama hiyo ni ajenda. "Sidhani kama hiyo ni ajenda, acheni maneno yasiyokuwa na maana, kila mtu ana marafiki, mbona hatuwaulizi, sidhani kama kuna tatizo." alisema kwa kifupi.
Hidden anger ...toward the reaction of the recipient.

]"Nachukia umaskini, napenda utajiri, natafuta uongozi wa nchi hii ili kuwasaidia Watanzania kuwa matajiri na si kukumbatia umaskini. Hii kudanganya watu kwamba nikiwa maskini ndiyo nafaa kuwa kiongozi ni ujinga ambao inabidi tuuache. Nataka watu wawe matajiri, tuache kuwabeza matajiri, matajiri wawe ni mfano kwa wengine, watu kama (Reginald) Mengi, (Said) Bakhressa na (Nazir) Karamagi wanatakiwa kuwa mfano kwa wengine, tungekuwa na watu kama hawa 20,000, nchi hii ingekuwa haikopi nje. Naukataa umaskini na nauchukia umaskini. Nakataa umaskini na ninataka watu wanihukumu kwa hilo," alisema.
Anger against his party policies and Ideology.
]Alipoulizwa kuhusu madai kuwa afya yake inaterereka, alisema anaamini yupo fiti na akashauri wagombea urais wote wakapimwe.
Anger against what the Public comments on his health status..as a public figure who his inteding to run for President Race 2015.

]"Sisi ni chama dola tumefanya mambo mazuri, lakini tusibweteke wenzetu wanajiandaa vizuri na sisi tunapaswa kujiandaa vizuri. Vyama vingi vilivyoleta ukombozi sehemu nyingi vimeshaondolewa mfano UNIP, Kanu na mkishaondolewa hamrudi madarakani, meseji yangu kubwa kwa chama changu tusifanye mchezo, tusibweteke badala yake tufanye kazi kubwa zaidi.".
Anger and Fear against other Political parties gaining momentum for the first office house plot position.

]"Hata nikikimbia kilomita 100 watasema mimi mgonjwa. Hivi karibuni nilitembea kilomita tano na albino jijini Dar es Salaam, kuna watu wakasema nimechoka sana, nimepata ‘stroke' na nimekimbizwa Ujerumani kutibiwa, huo ni upuuzi mtupu. Kuna chuki imeingia katika siasa zetu na kutakiana mabaya. Afya ni neema kutoka kwa Mungu tu. Napenda kuwahakikishia kuwa nipo fiti na nipo fiti na kwa lolote. Nadhani ni wakati sasa kwa chama chetu waweke utaratibu wanaogombea nafasi hii ambayo nitaitangaza Jumamosi, tukapime wote afya na mimi nitakuwa wa kwanza kujitokeza kwenda kupima.
Anger against those who speak to all issues related to his health state.
 
Back
Top Bottom