Ningekuwa mimi rais au msauri wake nisingeongelea maandamano ya CDM kwa sababu kuyaongelea ni kuyapa nguvu zaidi, badala yake ningesema serikali inafanya nini kupunguza makali ya maisha.we hushangai hadi kwenye hotuba ya raisi mandamano yanaongelewa!
Kuna kitu umekisema kimenigusa kwenye bold, hivi rais badala ya kushughulikia matatizo ya ndani yeye anashinda nje kusuluhisha migogoro ya wengine, kwanini asiwaachie kina Zuma ambao nchi zao hazina matatizo makubwa kama yetu? au yeye kaona sifa kama unavyosema kuonekana amepiga picha nchi za watu. Next utasikia amekwenda kusuluhisha mgogoro wa Libya.Walidhani ni chama cha msimu bila kujua cdm ni chama kinachofanya kazi msimu wote unaoufahamu, iwe wakati wa jua au mvua, kinauelewesha umma wajibu wake kwa serikali na kazi za serikali kwa umma. JMK anatishwa kwani hana anachoweza kufanya kuondoa shida za watz na sasa badala ya kuzunguka angani ili tusilale njaa anashinda hewani kupiga picha na wapinga demokrasia
Ningekuwa mimi rais au msauri wake nisingeongelea maandamano ya CDM kwa sababu kuyaongelea ni kuyapa nguvu zaidi, badala yake ningesema serikali inafanya nini kupunguza makali ya maisha.
Kuna baadhi ya wanasiasa na wanaJF walibeza maandamano ya Chadema kuwa hayatakuwa na impact yeyote, wengine wakadiliki kusema Chadema hawatapata watu Mwanza, lakini kadili siku zilivyoendelea yakatikisa anga lote la Tanzania hadi rais pressure ikampanda akaanza kulalamika kuwa kuna mpango wa kupindua nchi. Impact hiyo iliendelea kuwatoa watu ambao hatukutegemea kama kina Sophia Simba, Wasirra, Tendwa. Wengine tuliowasikia ni Fredrick Sumaye, Mzindakaya, Sitta, Lowassa nk. Hadi leo hii hata baada ya maandamano kwisha bado mtikisiko unaendelea kutikisa. Jana Pinda alipokewa na mabango yaliyoongelea maandamano ya Chadema. Hamuoni kuwa lengo la maandamano ya Chadema kisiasa limefikiwa. Nawauliza waliokuwa wanabeza wako wapi mbona hawaonekani tena au na wao wamekumbwa na impact ya maandamano, wanaona aibu.